Saturday, June 13, 2015

 Katika mwendelezo wa kumaliza kazi ya utume tuliyoachiwa na Mungu wa mbinguni.Sabato ya tarehe 13/06/2015, kanisa la Mbezi Luisi jijini Dar es Salaam liliichagua kuwa siku ya kuabudu pamoja na wageni kutoka sehemu mbalimbali, na hii ni kufuatia mafundisho ya nyumba kwa nyumba yaliyofanyika kwa majuma kadhaa katika maeneo ya jirani kuzunguka maeneo ya kanisa hilo.
Ibada kuu iliongozwa na mch. Enosi Mwakalindile aliyejenga somo lake katika kitabu cha Marko 8:34, HATUA ZA KUMFUATA KRISTO.
Na mwisho alitoa wito na watu 14 walijitoa kwa ubatizo na huduma hiyo ilifanyika na yeye mwenyewe kuwabatiza katika kisima kilichopo katika kanisa hilo.
Injilileo ilihudhuria na kuwa shuhuda wa tukio zima, na hizi ni baadhi ya matukio katika picha, KARIBU...
Kanisa lilijaa
Kwaya ya Kanisa la Mbezi Luis
Kwaya ya Vijana Mbezi Luis
Wabatizwa wakitoa ukubali wa viapo vya Ubatizo kwa kunyoosha mkono
Chakula cha mchana kilitangulia kabla ya ubatizo
Mch. Enosi Mwakalindile akiendesha huduma ya ubatizo
Watu wakishuhudia huduma ya ubatizo kama lilivyo agizo la Mungu wetu, atakayeamini na abatizwe kwa maji mengi.
Watu wakishuhudia huduma ya ubatizo kama lilivyo agizo la Mungu wetu, atakayeamini na abatizwe kwa maji mengi.
Foleni ya Wabatizwa kuingia kisimani
Timu ya Wainjilisti walioenda nyumba kwa nyumba wakionesha furaha yao kwa wimbo wa pamoja.
Baada ya ubatizo, zawadi zilifuata, Biblia na Vitabu viwili tofauti kwa kila mtu.
Mch. Enosi Mwakalindile akinena na watu
Tuwakumbuke katika maombi, maana wametangaza vita na shetani ,Mungu na awabariki nyote mliofanikisha haya yafanikiwe.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: , ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA