Wednesday, July 01, 2015

Ajali ililyotokea mapema leo asubuhi katika eneo la Kibaoni, wilayani Kilosa mkoani Morogoro ikihusisha basi la abiria aina ya Isuzu Coaster yenye nambari ya usajili T 837 CTM linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa Kilosa na Treni ya Abiria imesababisha vifo vya watu wasiopungua wanne (4) na majeruhi takribani 21.
Taarifa kutoka eneo la tukio limefafanua kuwa waliofariki ni wanaume wawili, mwanamke mmoja na mtoto wa miaka minne. Kwa upande wa majeruhi, majeruhi 21 wako wanaume 14 na wanawake 7 ambao wanaendelea na matibabu katika Hospital ya Wilaya ya Kilosa.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wiaya Kilosa, Dickson Masale amethibitisha kupokea miili ya watu watano akiwemo dereva wa basi pamoja na majeruhi 24.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 1 asubuhi na imetokana na uzembe wa dereva wa basi.
Picha na millardayo.com

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA