Wednesday, July 08, 2015

Katika nyakati hizi za Kizazi cha mwisho wa Dunia, kumezuka tofauti za IBADA zikisimamiwa na tofauti za Dini na Madhehebu. Neno la Mungu linasema: Waefeso 4:5 “BWANA MMOJA, IMANI MOJA, UBATIZO MMOJA”. Kuna Idaba nyingi tofauti zinazofanyika ambazo Shetani amezianzisha kwa siri akiwatumia viongozi wa dini bila kujua na kuwafanya wengi wamuabudu kama Mungu – 2Wakorintho 4:3-4, Warumi 1:24-27.Mungu anatoa wito wa mwisho kwa watu wote kutoka katika mifumo hiyo ya Ibada iliyo tofauti na Ibada ya Mungu wa Kweli – Ufunuo 14:6-7.

IBADA ya Mungu wa kweli ilianzishwa lini?

Neno la Mungu linasema IBADA ya Mungu Muumbaji ilianzishwa na Mungu mwenyewe siku ya SABA katika wiki ya Uumbaji Kabla ya Adamu kuanguka Dhambini – Mwanzo 2:1-4 Siku ya Saba katika wiki ya Uumbaji ndiyo siku ya Ibada – Aliibariki, Aliitakasa na Alipumzika, Kutakasa ni  kutenga kitu kwa Matumizi Matakatifu kama Mungu alivyoamuru – Siku ya saba inaitwa SABATO, sabato maana yake ni PUMZIKO.

Katika Vizazi vyote Mungu amewakumbusha wanadamu Kumuabudu yeye katika Siku hii ya SABA au SABATO ikiwa ni Ishara ya kuwa wanayemuabudu ni Mungu Muumbaji.

1. Kwa Mara ya kwanza Kabla ya Dhambi Adamu alimuabudu Mungu siku ya sabato – Mwanzo 2:1-4.

2. Waisraeli waliposahau kwa sababu ya maisha ya Utumwa kule Misri Mungu aliwakumbusha; Kutoka 20:8-11.

3. Ilikuwa Desturi ya Yesu kumwabudu Mungu katika siku ya SABATO – Luka 4:16

4. Mitume waliobaki baada Yesu kwenda Mbinguni walimwabudu Mungu katika Siku hii ya Sabato – Matendo 16:11-15, 13:42-44, 13:14, 18:4-11.

5. Mungu alimuonyesha Isaya kuwa, katika Nchi Mpya ambayo waliokombolewa wameandaliwa, isiyo na Dhambi, watakatifu watamwabudu Mungu Siku ya sabato kama ilivyokuwa katika Bustani ya EDENI kabla ya Dhambi – Isaya 66:22-24.

IBADA YA SIKU YA SABA - SABATO INA UMUHIMU GANI?

Ni ISHARA inayoonyesha kuwa Mungu anayeabudiwa ndiye Mungu Muumbaji, ndiyo pekee aliyoiweka kutofautisha na Ibada za Miungu Mingine ambayo haina uwezo wa Kuumba. Ezekieli 20:12, 20, Kutoka 31:12-18.

SIKU YA SABA AU SABATO YA KWELI NI IPI? NITAIJUAJE?

Wakristo wote duniani na wanahistoria wanakubaliana kuwa Yesu akufa siku ya Ijumaa na alifufuka siku ya Jumapili. Na katika historia Wiki au Juma la siku saba halijawahi kubadilika tangia uumbaji. Wanadamu wa kwanza waliitunza wiki kwa kuhesabu Moja hadi Saba, hivyo Sabato ndiyo iliitenga wiki.

Maandiko yanashuhudia kuwa Yesu alikufa siku moja Kabla ya Sabato yaani Ijumaa, siku ya Sabato wanafunzi wa Yesu walienda Kumuabudu Mungu wao na Siku iliyofuata yaani – Siku ya Kwanza au Jumapili – yesu alifufuka. Hivyo jumapili ni Siku ya Kwanza ya Juma. Marko 16:1-6, Mathayo 28:1-2, Luka 23:50-56, Luka 24:1-3.

Pia kitabu cha Mafundisho ya Kanisa kilichoandikwa: KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI ukurasa wa 484, inasema Jumapili ni siku ya Kwanza na ni Siku ya JUA, ila wakristo wanakusanyika kwa sababu ni Siku ambayo YESU alifufuka.

Nabii Mohamedi pia anathibitisha katika Quran kuwa wayahudi walioasi Amri ya Kuiheshimu JUMAMOSI walifanywa kuwa manyani wadhalilifu. Waisraeli walipaswa kutii maagizo ya waliyopewa na musa ili wawe kati ya wacha Mungu –

Soma Quran – Al Baqarah (2) : 63 na 64. 

NI NANI ALIIBADILI IBADA YA SIKU YA SABA (SABATO) KWENDA JUMAPILI SIKU YA KWANZA?

Vitabu vya historia vya Kanisa la Rumi lililohusika na Mabadiliko hayo vinathibitisha kuwa – Mfalme wa Rumi aliyekuwa anaitwa Konstantino, Ndiye aliyetoa Amri ya Kuiheshimu JUMAPILI kuwa siku ya IBADA kwa wakristo wa Rumi, Amri hiyo ilitangzwa Rasmi mwaka – 324 Baada ya Mitume wote Kufa, alipoongoka kutoka katika Upagani wa Kuabudu JUA, Ibada ya Jua ilikuwa inafanyika JUMAPILI – Siku ya Kwanza ya Juma. Soma Kitabu cha Historia cha kanisa la Roma – MIONZI

YA HISTORIA YA KANIS – Ukurasa wa 29 na 30, na THE COMPACT HISTORY OF THE CATHOLIC CHURCH – Page 22. Unaweza pia kusoma vitabu vya Historia za Ulimwengu.

IBADA YA JUA ya siku ya Kwanza au JUMAPILI – Ilianza zamani za kale enzi za Nimrodi, ilikuwa Ibada ya Kipagani ya Kumuabudu Mungu Jua badala ya Mungu Muumbaji. Mara nyingi shetani alitafuta njia ya Kuingiza kwa watu wa Mungu lakini Mungu aliipinga – Ezekieli 8:14-18, Kumbukumbu la torati 4:19.  

Kuna Sheria na Sabato za Kutoa Kafara – Hizi ziliisha baada ya Kifo cha Yesu Msalabani.


Na Mwinjilist: Eliezer Y. Mwangosi
Mobile Phone: 0767 210 299 
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA