Thursday, July 02, 2015

👉Tafakari: Mithali 31:10-12  "Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya,Siku zote za maisha yake."

Kati ya mambo yanayowashangaza wazazi wengi siku hizi ni kusikia, vijana wa kike wakisema hamna vijana wa kuwaoa wakati huohuo unakutana na vijana wa kiume wakihaha kutafuta mabinti wa kuoa, ukiwauliza, mbona mabinti wapo wengi? wanadai hamna wenye sifa za MKE MWEMA.

Yafuatayo ni baadhi tu ya mambo yanayowapotezea mabinti sifa za kufaa KUOLEWA:
👉UAMINIFU - Mabinti siku hizi utafikiri wana pepo la mapenzi, akiambiwa neno moja tu NAKUPENDA, ameachia kila kitu, utasikia vijana wanasema huyu "ni maharage ya mbeya, maji mara moja" au "Loose Ball" au "Cha wote" nk. Na vijana mara nyingi wanapenda kujaribu, akipata anawaambia na wenzie nao lazima waje kuonja. Kupata na kutoa mimba ni matokeo ya kutotulia, na mwisho ni kutozaa, ambalo ni changamoto ya kizazi chetu hadi vijana wanafikia kuzalisha kwanza ndio waoe.

👉KUPENDA MALI - Utasikia wanasema "Hapendwi mtu - PESA", wengi wanapeda waolewe na wenye uwezo, akisikia kijana ana Gari, masikio yote yanalegea. Mwishowe wanaishia kuchacha, wenye nazo wakiona binti anajigongagonga hawaachi, wanagonga na kuishia. Kurukia wenye nazo utaishia kuwa Kibanda hasara au banda la Uani. Mabinti mjithamini, nyie ni thamani sio wa kununuliwa kwa pesa.

👉KUTOKUWA NA KIASI - Wengi hupenda maisha ya juu "They are so expensive", wanatamaa na kupenda vitu vya gharama, kijana akipiga mahesabu anaona akikuoa yatakuwa maji marefu. Kupenda offer za gharama, kila mara kuomba vocha, hata uchumba haujakamilika, kila siku ni kutangaza mahitaji  - Vijana hawapendi kuombwa ombwa pesa. Pia Vijana wengi hawapendi Uzuri bandia wa Kujikoboa na make up zinazoharibu afya - Natural beauty is always Good, Ila uwe msafi na anayejipenda.

👉KUTOA HONGO YA NGONO - Wengi wanafikiri wakitoa huduma ya Ngono, ndio jamaa ataona anampenda kumbe ndio anaharibu, vijana wengi siku hizi wanadai hawaoni haja ya KUFUGA NG'OMBE WAKATI WANAPATA MAZIWA BURE. Mabinti wanaishia kuharibiwa na Kuachwa huku muda wa kuolewa ukiwa unayoyoma. Mabinti wote mkiamua kukomaa, msitoe huduma, vijana wengi wataoa.

👉KUTOJIAMINI - Wengi hawajielewi "Hawajisomi", Hawana maamuzi ya kwao, wanapenda kuiga, na kutegemea ushauri wa marafiki ambao mara nyingi wanawapotosha kwa sababu ya wivu. Unakuta kila anayekuja anamrukia, hawana msimamo, binti anakuwa na wachumba watano, wa outing au kujirusha, wa kanisani, wa ofisini kwa ajili ya offer, n.k. BINTI unapaswa Kujiamini, Omba Mungu pata ushauri kwa wazazi halafu toa majibu sahihi kwa wakati. Ndoa haina "Copy and Pest".

👉 Pia kuna vikwazo vya wazazi na juu ya kupangiwa Mahali kubwa kama wanauza trekta, nitayaongea katika mada nyingine ya wazazi na vijana, nalo ni tatizo sugu siku hizi. Hata hivyo binti hatakiwi kuanza mahusiano yoyote ya uchumba bila kupata ushauri wa wazazi au walezi. BINTI USITOE JIBU LA NDIO KUANZA UCHUMBA BILA USHAURI kutoka kwa wazazi au walezi, utaishia kubwagwa.

BINTI Mtumaini Mungu, kwake yote yanawezekana, bila kujali ulikosea wapi, Umetelekezwa, Umri umekwenda, kwa hali yoyote uliyonayo, Mungu yupo kwa ajili yako, atafanya njia pasipo njia, tulia miguuni pake, ngojea AHADI NAYE ATATENDA.

WOTE WAZAZI KWA VIJANA NAWATAKIA MAISHA YENYE FURAHA NA BARAKA TELE

Na. Ev.  Eliezer Mwangosi - 0767210299,  Email - eliezer.mwangosi@yahoo.com


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA