Monday, November 23, 2015

Katika ibada ya Sabato ya tarehe 21 kanisa la Ilala SDA la jijini Dar es Salaam limeweka wakfu kwa Mungu  vyombo vipya vya mawasiliano, ikiwemo Mixer kubwa yenye njia 24, Spika kubwa 2, Spika ndogo 2, Amplifaya 1, Snake Cable 1.

Awali akitoa taarifa ya kile kilichonunuliwa, mkuu wa mawasiliano kanisani hapo Bwana Elishama Marwa alisema wanashukuru kwa upatikanaji wa vifaa hivyo ila bado wanahitaji kubwa la vifaa vingine kama Vipaza sauti na stendi zake hivyo kutoa wito kwa watu wengine kujitokeza kusaidia kuondoa hitaji hilo.

Mchungaji wa kanisa, Mch. Shehemba katika huduma yake ya kuviweka wakfu vifaa hivyo alikazia kuhusiana na matumizi ya vifaa hivyo ya kwamba ni kwa ajili ya Mungu pekee hivyo kuwaomba waangalizi wa vifaa hivyo hasa idara ya mawasiliano kuwa makini sana na matumizi ya vifaa hivyo.

Timu ya injilileo, tunawapongeza kwa hatua hiyo na kuwaombea kwa Mungu vifaa hivyo vitumike kama ilivyokusudiwa kwa kusudi la injili.
Mixer ya zamani ikiwa katika matumizi ya sabato hiyo
Kijana Samwel akipiga kinanda katika Ibada
Viongozi wa Idara ya mawasiliano kanisani wakiondoa vitambaa kuwaonesha washiriki vifaa vilivyonunuliwa na hatimaye kukabidhiwa kwa Mungu
Vifaa vilivyonunuliwa katika awamu ya kwanza
Kiongozi wa Mawasiliano Elishama Marwa akitolea maelezo vifaa vilivyonunuliwa na nyuma yake ni Mchungaji wa kanisa Sadickiel Shehemba
Kiongozi wa Mawasiliano Elishama Marwa akitolea maelezo vifaa vilivyonunuliwa na pembeni yake ni Mchungaji wa kanisa Sadickiel Shehemba
Mchungaji wa Kanisa Sadikiel Shehemba
Mchungaji akianza Huduma maalum
Monitor Speaker
Maombi yakiendelea

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA