Tafakari: Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo mtazidishiwa".
Kila kunapokucha maisha ya mwanadamu yanazidi kukutana na changamoto za kukatisha tamaa. Kuanzia maisha ya mtu binafsi, familia, taifa hadi mataifa n.k. Kila siku zinaibuka changamoto mpya zinazoumiza vichwa.
Bila kujali; uzuri wa maumbile, hali ya kifedha, elimu waliyonayo, mali wanazomiliki, demokrasia walizonazo, uwe katika ndoa au laa, uwe na mchumba au katika mahusiano yoyote, mwanadamu awe na hali yoyote ile, ni hakika anayo changamoto, na kama kwa sasa hana; atakuwa amaisha ipitia au ziko mbele zinakuja.
Sikiliza; Watu wanatafuta AMANI, lakini Kila leo amani inazidi kupotea, wengi wanatembea wakiwa na maumivu moyoni, kila mmoja akiwa amejeruhiwa na jambo fulani. Hata siku hii leo wengi wana mizigo mizito, hawajui mwisho wake. Vijana wana changamoto, watu wazima ndio usiseme, viongozi wa mataifa makubwa kwa madogo hawalali.
Hitaji letu kuu ili kupita salama katika dhoruba hizi za ulimwengu ni kumrudia Mungu, kuutafuta ufalme wake kwanza, adha zote tunazozipata ni mishale ya adui shetani, inayotupata kwa HILA. Amani ya kweli na ya kudumu bila Mungu, ni kujilisha upepo. Wanaodai wana amani bila Mungu, hiyo ni ya kitambo tu.
Ayubu 22:21 inasema "Mjue sana Mungu, ili uwe na AMANI; ndivyo MEMA yatavyokujia". Hakuna njia ya mkato ya kupata Amani ya kweli nje ya kutoa maisha yetu kwa Kristo, aliyekuja kumuokoa mwanadamu, na kumuweka huru na mishale ya Adui shetani, ambayo ni dhambi na matunda yake.
MUNGU ATAWALE NIA YA KILA MMOJA WATU ILI TUPATE USHINDI MILELE.
NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE AMANI NA BARAKA TELE.
Na Ev. Eliezer Mwangosi.
MUNGU ATAWALE NIA YA KILA MMOJA WATU ILI TUPATE USHINDI MILELE.
NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE AMANI NA BARAKA TELE.
Na Ev. Eliezer Mwangosi.
0 comments:
Post a Comment