Washiriki wa Mwenge nawasalimu katika jina la BWANA.
Sabato ya tarehe 19 December 2015 (Sabato ijayo) ni Sabato ya Majengo, kwa niaba ya kamati ya upanuzi wa jengo la Kanisa Mwenge, nawasihi kila mmoja apange kupunguza au kukamilisha kabisa ahadi yake ya upanuzi wa jengo aliyoitoa tarehe 3-10-2015 ili tuweze kukamilisha awamu ya kwanza ya upanuzi ifikapo December 31 2015. Siku hiyo itatumika kuhamasisha ukamilishaji wa ahadi tulizotoa na kwa wale ambao hawajatoa waweze pia kutoa. Kamati inawashukuru wote kwa kujitoa kwenu katika kazi hii, shukrani pia kwa wote ambao wamekwisha kukamilisha ahadi zao, waliopunguza na wanaoendelea kupunguza nadhiri zao. Tunatoa wito kwa kila mshiriki, mshiriki wa shule sabato na mgeni unayekuja kuabudu nasi ushiriki katika kuwezesha kazi hii isonge mbele.
Uchangiaji wa upanuzi huu ni endelevu hadi jengo litakapokamilika kama tunavyokusudia ifikapo December 2016. Taswira ya mwonekano wa jengo litakapokamilika imeboreshwa zaidi na sasa itakuwa ya kisasa zaidi au kwa kiingereza "Contemporary Design" kama inavyoonekana katika picha hapo chini.
Usomapo ujumbe huu mtumie na mshiriki mwingine unayemfahamu kwa fb au whatsapp yake.
Ubarikiwe unapopanga kutimiza nadhiri yako kwa BWANA Sabato ijayo.
UMOJA NI NGUVU, KWA PAMOJA TUNAWEZA.
HAPA KAZI TU (YA KUMWINUA MUNGU)!.
Habari/Picha Zakaria Ngeleja
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment