Ukijaribu kukumbuka matukio makubwa yaliyoingia kwenye kumbukumbu za watu wengi Jumapili ya tarehe 20/12/2015, moja wapo ni tukio la Sherehe ya harusi ya Bw. Yared Omolo na Bi. Penina Moses.
Ilianza katika bustani nzuri katika hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es Salaam, ambapo msajili wa ndoa kutoka ofisi za wilaya ya Ilala aliwaunganisha wawili hawa waliosindikizwa na ndugu, jamaa na marafiki kuwa mke na mume na baadaye tafrija ya kuwapongeza katika ukumbi wa Bahari ulio ndani ya hoteli hiyo ya Lamada.
Wasiowafahamu maharusi hawa, kwa ufupi Bwana harusi amekuwa maarufu sana kupitia huduma yake ya uimbaji katika nyimbo za injili kwa muda mrefu sasa katika jiji la Dar es Salaam wakati pia Bibi harusi ni muimbaji. Yared, ni muimbaji wa kwaya ya kanisa la Waadventista Wasabato Ilala na kikundi cha uimbaji cha Holy Reunion wakati huo Penina ni muimbaji pia.
Injilileo ilikuwa shuhuda wa tukio hili hadi mwisho na hapa tupo tayari kukuonesha matukio katika picha yaliyojiri tangu mwanzo hadi mwisho.
Tunapenda kuwapongeza sana kwa hatua hii, tunawaombea heri na baraka katika ndoa yao.
|
Bw. Yared akitoa kiapo kwa Bi. Penina |
|
Bi. Penina akitoa kiapo kwa Bw. Yared |
|
Akipokea hati ya ndoa |
|
Kwaya ya kanisa la Wasabato Ilala wakiimba wimbo wa pongezi baada ya kuunganishwa |
|
Kikundi cha Holy Reunion wakiimba wimbo wa Pongezi |
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment