Thursday, December 03, 2015

TANGAZO
Ofisi ya katibu mkuu wa unioni konferensi ya kaskazini mwa Tanzania, inapenda kuwakaribisha katika semina ya mafunzo maalumu ya mfumo mpya wa kutunza kumbukumbu na usimamizi wa makanisa ya Waadventista wa Sabato unaofahamika kama ADVENTIST CHURCH MANAGEMENT SYSTEM (ACMS)
Mafunzo yatatolewa tarehe 08 - 10 Desemba 2015 katika kanisa la Waadventista wa Sabato Njiro Mkoani Arusha.
Makundi yafuatayo yanapaswa kuhudhuria:
1. Makarani wote wa makanisa mahalia katika unioni2. Wanateknohama(IT) wote katika makanisa mahalia
3. Wanateknohama( IT) wote wa Konferensi na taasisi za kanisa
4. Wachungaji wote wa mitaa
5. Wakurugenzi wote wa Idara ya mawasiliano katika unioni, konferensi na Taasisi.
6. Wasaidizi wote wa Makatibu wakuu wa unioni na konferensi,
7. Makatibu wakuu wa unioni na konferensi.

Wakufunzi:
1. Sherri Ingram - Mkurugenzi wa mfumo wa usimamizi wa kumbukumbu za kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni.
2. Tom Ogal - Msaidizi wa Katibu Mkuu kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
3. Haggai Abuto - Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kanda ya Afrika mashariki na Kati
Gharama zote za chakula, malazi, usafiri na bima zitakuwa chini ya kanisa au ofisi inayotuma mjumbe.
Tarehe ya kuwasili ni 7 Desemba 2015 na tarehe ya kuondoka ni 11 Desemba 2015.
Fomu ya usajili inapatikana kupitia http://bit.ly/2015NTUCACMSTraining
Barua rasmi ya mwaliko na ruhusa inapatikana kupitiahttp://bit.ly/2015ACMSTraining
Ni muhimu kila kanisa na ofisi za kanisa kutuma mjumbe ili kujifunza mfumo mpya wa kutunza kumbukumbu za kanisa na usimamizi wa makanisa ya Waadventista wa Sabato
Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu
Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania
+255 784 388190
acms@ntucadventist.org

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA