➡Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. 2 Petro 3:17.
1 Katika siku hizi za mwisho, maovu yanapozidi kuongezeka, na upendo wa wengi unavyozidi kupoa, Mungu atakuwa na watu wake watakaolitukuza jina lake, na kusimama kama wakaripiaji wa dhambi. Wanatakiwa kuwa "watu wa pekee," ambao watakuwa waaminifu kwa sheria ya Mungu [Amri Kumi], wakati ulimwengu utakapojaribu kuzitangua amri zake; na wakati uweza wa Mungu unaoongoa utakapofanya kazi ndani ya watumishi wake, majeshi yale ya giza yatajipanga na kutoa upinzani mkali sana, uliodhamiriwa. Shetani atafanya kazi yake kwa "uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo, na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea." Atatumia kila mbinu ya udanganyifu kuishawishi mioyo ya wanadamu....
2 Kazi hiyo ya uasi huanzia katika maasi fulani ya kisirisiri ndani ya moyo wa mtu dhidi ya matakwa ya Sheria ya Mungu. Tamaa chafu, tamaa isiyo halali ya kupenda makuu, hutunzwa na kuendekezwa moyoni, na mashaka na giza humtenga mtu huyo mbali na Mungu. Tusipoyashinda maovu hayo, yatatushinda.
3 Watu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisonga mbele katika njia ile ya kweli, watajaribiwa kwa maonjo na majaribu. Wale wanaosikiliza mashauri ya Shetani, na kukengeuka kutoka katika unyofu wao, wataanza kwenda katika njia ile inayoshuka chini, na jaribu fulani lililoandaliwa [na Shetani] kwa werevu sana litawaharakisha kwenda kwenye njia ile ya uasi, mpaka kushuka kwao kutaonekana dhahiri na kunakuwa kwa kasi sana. Dhambi zile zilizokuwa za kuchukiza mno kwao hapo kwanza, [sasa] zinakuwa za kuvutia sana, nazo hukaribishwa na kutendwa na wale waliotupilia mbali kicho chao kwa Mungu pamoja na utiifu wao kwa sheria yake. Lakini furaha yao nyingi sana mwanzoni mwa uasi wao, itaishia katika majonzi, kujivunjia heshima [aibu], na maangamizi.
4 Tunahitaji kuwa macho daima, kukesha na kuomba ili tusije tukaingia majaribuni. Kujiendekeza kuwa na kiburi cha kiroho, tamaa mbaya, mawazo machafu, na cho chote kile kinachotutenga mbali na ushirika wetu wa karibu sana, ulio mtakatifu, pamoja na Yesu, huziweka roho zetu katika hatari kubwa. Yatupasa kuwa na imani iliyo hai kwa Mungu.... Kama wazo hilo la uasi linawasikitisha ninyi, nanyi hamtaki kuwa maadui wa ile kweli,... basi, "lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema." Warumi 12:9.
BARAKA ZA BWANA ZIAMBATANE NA KILA MMOJA WETU KATIKA SIKU YA LEO.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment