Friday, January 01, 2016

Tafakari: 2 Wakorintho 5:17. "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita ; tazama! yamekuwa mapya".

Kila mtu akipewa nafasi ya kuelezea hali ya maisha aliyoipitia ndani ya mwaka mzima wa 2015, kuna mengi tungeyasikia, mengine yatakuwa ya kufurahisha, mengine ya kusikitisha, mengine ya kukatisha tamaa n.k. Kila mtu amepitia hali fulani iliyo tofauti na mwenzie. Hata hivyo kwa neema ya Mungu yeyeto aliyefanikiwa kuusoma ujumbe huu, hana budi kumshukuru Mungu kwa kupatiwa nafasi tena kuuona mwaka 2016. 

Kuna watu mwaka 2015 umepita kama wako peponi, kila waliyoyapanga yalienda salama na afya zao zikiwa bila migogoro. Wengine hali zao zilikuwa nusu nusu, mara wako peponi mara majonzi. Kuna wengine mwaka mzima umekuwa majanga matupu, machungu yamekuwa mazito kiasi cha kutoona mazuri. Kuna watu wamejeruhiwa na kubaki mioyo yao ikiwa imejaa majeraha ambayo hawana matumaini ya kupona. 

Mpendwa; haijalishi umepitia maisha gani mwaka ulioisha, iwe ni furaha na baraka tele au maumivu ya kukatisha tamaa, haijalishi hali ya machungu ilipita au inaendelea, ziwe ni changamoto za magonjwa, iwe ni kuporomoka kwa biashara, iwe ni upweke, iwe ukata wa pesa, iwe ni kukosa ada ya shule au chuo, iwe ni kusalitiwa na umpendaye, iwe ni changamoto ya kisiasa kukosa cheo, iwe ni kuonewa, iwe ni kupitiwa na mikasa ya Rushwa n.k. Neno la leo linasema ANZA UPYA NA BWANA. 

Siri ya mafanikio na kuwa na maisha yenye matumaini milele, ni kuwa mikononi mwa Mungu. Hata dhoruba za maisha zikivuma, ndani ya Kristo ni salama. Kumbuka rafiki, maisha bila Mungu ni kujilisha upepo, utajiri na ukuu wa dunia hii bila Yesu ni maisha ya kubahatisha.

Amua sasa kuanza upya na Bwana, na hatimaye ukiri na kusema - YA KALE YAMEPITA, TAZAMA YAMEKUWA MAPYA. 

NAWATAKIA MWAKA MPYA WENYE BARAKA TELE ZA MUNGU NA MAISHA YENYE MATUMAINI. 

Na. Ev. Eliezer Mwangosi - Simu: 0767210299.



****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA