Wednesday, January 06, 2016

Tafakari: Warumi 2:4 "Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? "

Jambo la hatari ambalo adui shetani amelifanya katika ufahamu wa watu, ni kuwaaminisha kuwa Mungu anachukuliana na Dhambi, na hasa wanapoona maisha yanasonga huku wakidumu kuishi maisha ya Dhambi. Ndio maana tulishuhudia vituko vingi wakati wa sikukuu na mikesha ya Krismasi na Mwaka mpya. 

Katika siku ambazo zilipaswa kumshukuru Mungu, kwa kuwapatia uzima, wengi waligeuka wakamdhihaki Mungu kwa kutenda maovu. Ndivyo ilivyo kwa wengi wanaojiita watoto wa Mungu au wacha Mungu, wanahudhuria majumba ya Ibada, huku mioyo yao haiko tayari kuachilia dhambi ambazo ni dhahiri, japo zinafanywa kwa siri. 

Mpendwa; ukiona kuna dhambi unaitenda na unajiona uko salaama, wala moyo wako haukusumbui juu ya dhambi hiyo, jua uko katika hatari ya kumkufuru Roho mtakatifu na hatimaye kupotea milele. Wakati wote Mungu anasumbuka kumvuta mdhambi ili ATUBU, Je ni wangapi wanachukua hatua ya KUTUBU na kuacha? 

Neema ya Mungu ikawe juu ya kila mmoja, ikizidi kutupatia NURU zaidi, kwa ajili ya kuishi maisha ya ushindi katika Kristo Yesu, ambaye katika yeye tunapata wokovu na kujitenga na maisha dhambi. 

NAWATAKIA MAFANIKIO NA BARAKA TELE TUNAPOENDELEA NA MWAKA MPYA. 

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA