Friday, January 22, 2016

Tafakari: Malaki 2:15-16 "..... Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA...."

Hili ni agizo la Bwana kwa wote walio Katika NDOA, walio katika fungate la Uchumba, wanaotafuta wachumba, na wale ambao tayari wameachana. Kuachana ni dhambi inayomchukiza Mungu, kizazi chetu kimejaa wahanga wa dhoruba hii ya kuachana kwa sababu ya Ndoa nyingi kuanzishwa katika misingi mibovu. Sababu nyingine ni wanandoa kutojisalimisha kwa Mungu ili atawale muungano wao. 

Ndoa ni taasisi iliyoanzishwa na Mungu kabla ya dhambi,  ipo kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ndoa kwa asili ni muungano wa kiroho kati ya watu wawili, kwa ajili ya kuwa mawakili wa Mungu. Ndio maana shetani anapiga vita, na kurusha mishale yenye sumu za kila namna, kuhakikisha ndoa zinakuwa ndoano, au zisitimize kusudi la Mungu. 

Ninawaasa vijana, mruhusu Mungu awaongoze na kuwapatia wenzi wema, acheni kurukia rukia, na kudakwa dakwa kama mipila, acheni kuwa na wachumba mnawaowakubali huku mnao wengine, acheni udanganyifu, UPENDO na uwe wa kweli uliojengwa na Mungu. 

Wenye ndoa, bila kujali mwanzo wenu, salimisheni ndoa zenu kwa Mungu, ili azilinde na mishale ya Adui. Wale wanaopanga kuwasaliti wenzi wao, kwasababu zozote zile wasifanye hivyo. Mruhusu Mungu aingilie kati kila changamoto, kwake yote yanawezekana. 

Walio watelekeza wenzi wao na kujiegesha kwa vijumba hasara, bila kusahau ma suger mam, wanao hujumu ndoa zao kwa kufuga vi serengeti boys,  waache mara moja kabla hasira ya Bwana kuwaka juu yao na kulipa kisasi. 

NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO NA BARAKA TELE. 

Na. Ev. Eliezer Mwangosi - 0767210299.


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA