Kutoka 14:14 “Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.”
Magumu yatakapowakuta maishani na kuwa kama mlima usiopenyeka, siri pekee ni kukaa kimya mbele ya watu na kuufungua moyo wako kwa Mungu kwa sababu kutulia ni tiba ya matatizo. Imeandikwa katika Isaya 30:15 “Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.”
Ndugu na dada ingekuwa vyema asubuhi hii ukayatoa maisha yako kwa Mungu ili ayaongoze. Mtwisheni yeye fadhaa zenu zote naye atawabebea. 1 Petro 5:6 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.” Mungu awabariki mnapofanya hivyo, katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Amina.
CHANZO STEPHEN LETTA
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment