Monday, March 14, 2016

 Aliyekuwa Mchungaji wa Mtaa wa Kimara, Mch. Rahis Mande ameagwa mapema jumamosi hii katika siku ya kuabudu ya Sabato na kumkabidhi Mchungaji mpya kwa mtaa huu ni Mch.James Machage ambaye hakuwepo kwenye hafla hii fupi kwani alikuwa na dharura.
Mbali na risala iliyotolewa toka kwa uongozi wa kanisa, hatimaye Mchungaji Mande ambaye ni Mchungaji wa Mtaa wa Magomeni kwa sasa, nae alipata kuongea huku akitokwa na machozi kwani aliweza kuishi vyema na washiriki wa mtaa huu wa Kimara, aliwashukuru na kuwaomba kutoa ushirikiano huo pia kwa Mchungaji mpya kwa mtaa huo.
Kulia ni Mchungaji Mande alipokuwa akipokea zawadi toka kwa mshiriki wa Kanisa na kushoto ni mke wa Mchungaji.




 Picha/habari na KIMARA SDA CHURCH WEBSITE
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA