Friday, April 01, 2016

 1Wakorintho 11:23-39 "Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,  naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.

TAFAKARI:
Mbali na Sherehe ya Easter ambayo wakristo wengi wanasherekea kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ndani yake imeunganishwa na huduma takatifu ya Pasaka ambayo wengine wamezoea kuita Meza ya Bwana.

Bahati mbaya sana, kwa kutokujua, wengi wamelichukua jambo la pasaka kimwili bila kupambanua mambo halisi ya uzima wa milele. Wengi wanajipatia hukumu za nafsi zao badala ya kuuthibisha wokovu wao.

Yesu aliacha kielelezo cha kuadhimisha pasaka, ambacho ndicho mtume Paulo anaeleza namna ya kushiriki, ili pasaka iwe na maana mbali na LAANA, mkristo lazima ajihoji na kupambanua maisha yake, asalimishe maisha yake kwa Kristo kwa ajili ya Utakaso kabla ya kuadhimisha pasaka.

Kuna Giza nene linazidi kufunika ukristo, kwa watu wengi kuifanya sherehe hii kuwa ya kunywa na kula na kukidhi tamaa za miili yao, jambo la kushangaza utakuta hata wengine waliokuwa wamefunga kwaresma, siku ya Pasaka ndiyo ya kufidia yote hadi Ulevi na kujistarehesha na anasa zingine za kidunia.

Pia kuna watu wengine ambao hawaelewi kuwa sherehe ya Easter haina maana ya adhimisho la Pasaka ya kwenye biblia, hivyo kuishia kufanya sherehe bila kushiriki huduma ya kiroho ya meza ya Bwana (Kumega mkate na Divai), hizo zinakuwa ni burudani za mwili tofauti na agizo la Kristo. 

Kwa mazoea hayo wanadumu kubaki MAKABURINI wakati Yesu ameimaliza kazi ya kuwafufua kutoka MAKABURI ya Dhambi, hivyo wakati wanasherekea kufufuka kwa Yesu wanakuwa pia wanasherekea mauti yao ya milele.  Hebu kila mmoja ajihoji, maisha yake Kabla na Baada ya pasaka yakoje.

Mtume Paulo kwa Waebrania anasema; "...Wanaotenda dhambi baada ya kuufahamu ukweli... WANAMSULUBISHA mwana wa Mungu Mara ya pili kwa nafsi zao na KUMFEDHEHI kwa dhahiri. Soma na kutafakari - Waebrania 6:4-6, 10:26-27.

NENO LA LEO, litusaidie kupambanua maadhimisho yetu ya pasaka, ili yawe ya Baraka badala ya laana katika siku zetu zilizobaki za maisha haya, kusiwe na atakayepotea kwa kutokujua. Kila mmoja ajiangalie, ikiwa mmoja wetu bado yuko kwenye dhambi fulani; wakati alishiriki pasaka; anapaswa kuacha haraka, aungame na kutubu na kujutia moyoni, kwa kumdhihaki mwana wa Mungu na Kafara aliyoitoa kwa ajili yake.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA NA FURAHA TELE NDANI YESU KRISTO.

Na: Eliezer Mwangosi - 0767210299
.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA