Tuesday, May 31, 2016

 Zaburi 137:3-4 "Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni?".

Mara nyingi waisraeli walipokuwa wanachukuliwa mateka, walikuwa wanaombwa kuimba nyimbo walizokuwa wakiziimba walipokuwa kwao katika Ibada za Mungu wao.

Walitaka wawaimbie kwa ajili ya dhihaka, juu ya Yehova, katikati ya sherehe za Miungu yao. Izraeli walitundika vinubi vyao na kuhoji - Tuimbeje wimbo wa Bwana katika nchi ya Ugeni? .

Nakumbuka kisa kilichotokea kwa wainbaji waliokuwa katika huduma ya Injili, jioni walipomaliza kuimba, mwalimu wa kwaya na mwimbaji wa kike kinara wa sauti ya kwanza, walitoroka wenzao na kwenda guest house kwa ajili kujipa maraha.

Kabla ya yote wakiwa chumbani,  mwalimu akaomba aimbiwe wimbo akiwa amempakata, kwani alijisikia raha akisikia sauti ya binti ikiimba. Alipoanza kuimba, kabla hajamaliza mstari, akadondoka chini huku damu ya hedhi ikibubujika mithili ya bomba la maji.

Ikawa ndio mwisho wa starehe, binti akakata roho, mwalimu wa kwaya akashikwa na kuwekwa ndani kuisaidia polisi, huku huduma ya Injili ikiwasubiri pasipo mafanikio - zikatimia za mwizi arobaini.

Kuna vijana wengi wa kike na wa kiume na hata wazee, wanamdhihaki Mungu, wanaimba nyimbo za kumtukuza Mungu, huku wakivinjali na mahusiano ya mapenzi. Kuna baadhi ya wanakwaya, mashemasi, wachungaji, wazee, wainjilisti, manabii na mitume, ambao wako katika utumwa wa Zinaa na Uasherati.

Kila anayejiita mtumishi wa Mungu; akifanya dhambi kusudi, ni sawa na kuimba wimbo wa Bwana katika nchi ya Ugeni, kwa ajili ya shetani na mizimu kumdhihaki Yehova. Soma: Waebrania 6:4-6, 10:26-27. Kutenda dhambi kwa Mkristo ni Kumsulubisha na Kumfedhehi kwa dhahiri.

Wakati shetani akizidi kushangilia, kwa kuwa na waimbaji wengi, wakiwa upande wake wakiimba nyimbo ugenini, bila hata kujali; wito unatolewa tena, wa Kurudi nyumbani. TOKENI KWAKE ENYI WATOTO WA MUNGU, Kabla ya siku ya kisasi cha BWANA. Huu ni wakati wa Kusema Bye Bye shetani, kwa Jina ya Yesu.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO TELE.

Na Ev. Eliezer Mwangosi

Simu no. 0767 210 299.




****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA