Sunday, May 15, 2016

Nimealikwa mwezi ujao arusi ya watu wenye uwezo wa Kanisa la Baptisti hapa Marekani. Wameniambia nije na chakula changu (potluck). Wameniomba ama niwasaidie chakula, au nije kupika, ama nilete matunda, na nije kusaidia kupanga viti. Hawa ni wazungu wenye majumba makubwa ila wanawiwa na utumishi wa kujinyima kwa ajili ya watu wengine.
Mwaka juzi wamerithi watoto wawili kutoka Uchina, na wana mpango wa kuwachukua wengine maana wamesema hiyo ndiyo njia yao waliyoamua kutumia ili kuwaongeza watu hao kukutana na Kristo! Kwa kweli huwa najiuliza haya magauni aghali ya harusi tunayonunua kwa ajili ya siku ya harusi, baada ya siku ile huwa tunayapeleka wapi? Si nafuu hata ya suti unaweza kuendelea kuivaa hata baada harusi.
Nina vibibi [hapa Marekani] vingine vizee vimekuwa vikinipa magauni yao ya arusi yana miaka 40! Kuna msemo mmoja watu husema kwamba sisi binadamu wote tuna tabia ya kutumia pesa kwa vitu tusivyovihitaji, ili tu kupendezesha watu tusiowajua kwa pesa tusiyokuwa nayo (We want to spend the money we do not have, to impress the people we do not know, with the money we do not have).
Hii tuichukue kama changamoto ya uwakili ya kila mmoja wetu kila kukicha. Nakumbuka Mama Twing mmishonari [aliyekuwa na makao yake kule Kigoma] nilipomwona mara ya kwanza Youth congress ya 1988 mjini Dar es Salaam wakati alipotutembelea kwetu Mzazi wangu akasema "Huyu [mzungu] anatembea na nguo zake za 'kauka nikuvae nzuri tu mbili hivi. Hajionyeshi ingawaje ni mtu mwenye pesa, na ana watoto wanaofanya kazi nzuri na mume aliacha kiinua mgongo kizuri naye pia amesoma vizuri !"
Siku nyingine tukamtembelea Barry Mosier [mzungu mwingine] kule Kibidula. Mzazi wangu alipomwona na mkewe wakimshugulikia mtoto mwathirika akiugua kuharisha na mengineyo aliniambia kwa faragha "Kweli hawa ndiyo watu wa Mungu si mimi na wewe?!" Nikamwambia kwani vipi, akasema mtoto anaharisha mchanga, nao watoto wao wamekuwa wakubwa na wanapoteza pesa kila mara wanamnunulia hichi sisi tunaenda kanisani na kuimba nyimbo mbili tatu na kula potluck na kufuta mdomo tunajiendea nyumbani.
NIlicheka ila nimekuwa nikijifikiria toka siku ile kwamba mambo mengi hayafanyiki kwa "Nia ya Yesu au Ubongo wa Yesu" Filipi 2:5 HIi Mind set of Jesus au Frontal Lobe of Jesus ni kitu cha kuombea kila kukicha, maana ndani ya moyo jambo la kujionyesha lipo kwa kila mtu na hivyo yale mashauri ya Wafilipi hayapewi nafasi. "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo." (Wafilipi 4:8)


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA