Wednesday, June 22, 2016


Usije ukadanganywa kwamba waliokufa wanaweza kuombewa baada ya kufa ili uende kwa Mungu. Mimi na wewe kila mmoja amepewa nafasi moja ya kuishi na tena baada ya kuishi ni hukumu itafuata ya yale tuliyoishi kwayo.
Maisha yako yatadhihirisha kwamba umemchagua Mungu au shetani. Kumchagua Mungu kunatutaka kukimbia kila aina ya uovu na kutenda tu yaliyo ya haki na upendo. Kumfuata shetani hakututaki kuacha mema yote. Hata kama unatenda mema yote lakini kwa jambo moja unadumu na kung'ang'ania kulitenda unakuwa umejisalimisha kwake. Wakati ambao Mungu anataka tujitenge na uovu wote lakini shetani hataki tujitenge na uovu wote ili tuwe wake. Hilo ovu moja unaloendekeza linampa shetani nafasi ya kukushitaki na kukutwaa kama mali yake.
Mungu amempatia kila mtu uhuru wa kuchagua. Mungu anapendezwa na wale wanaomchagua kwa hiari yao. Waliokufa hata hivyo hawawezi kuchagua.
Mathalani mimi nikishakufa msinililie wala kuniombea. Kama unanijali nijali sasa nikiwa hai na ufahamu. Niombee sasa kwamba niyatende mapenzi ya Mungu. Lia kwaajili ya yeyote anayeendekeza uovu na mweleze uovu wake. Akiacha uovu huo, umompata ndugu yako. Akiendekeza uovu msii na kumwombea mpaka atakapokufa. Akifa katika uovu UMEMPOTEZA. Sitaki kuwa mnafiki. Mbinguni watakwenda wale waliomchagua Mungu kwa hiari yao. Uchaguzi wangu na wako ni kabla ya mauti.

Kuombea maiti ni upagani. Nadhani sijaeleweka. Kuombea maiti ni UPAGANI na tena Ibada ya mizimu. Kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu. Kuomba maiti vivyo hivyo. Hata kama uliwahi kuombea au kuomba maiti au mfu acha mara moja. Kwa kufanya hivyo unajifungamanisha na mashetani.
👓kuombea au kuomba wafu siyo fundisho la Biblia, 👓kuombea au kuomba wafu ni upagani 100%
Hiyo basi tengeneza mambo yako ili kifo kikukute ukiwa umejiimarisha mikononi mwa Muumba wako.
Mungu akubariki. Jioni njema






****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA