Thursday, June 30, 2016

Yohana:14:27 "Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga."

Siku moja nikiwa nasafiri kwa basi, nilikaa karibu na mama mmoja, mara baada ya muda mfupi nikasikia simu yake inaita, alipoipokea akaanza kuporomosha matusi kwa kufoka, huku akifyonya. Muda haukupita nikamuona anaanza kulia. Ilibidi nitulie na kuanza kumuombea kimoyomoyo, ili Bwana atulize dhoruba iliyo katika moyo wake, make niliona akiwa na stress kubwa.

Baada ya nusu saa kipita alionekana kutulia, ndipo nikaamuliza lililomsibu, akaongea kwa jazba akasema "Si MBWA huyu anautesa moyo wangu!" Kupitia maelezo yake niligundua mume wake hakulala nyumbani, alipitia kwa Mchepuko hadi asubuhi. Mke wake alionyesha hali ya kuchoshwa na kuumizwa kwa usaliti wa mapenzi, kiasi kwamba kila siku alikuwa na stress au msongo wa mawazo.

Kadiri siku zinavyosonga, ndivyo idadi ya watu wanaoishi na misongo ya mawazo inavyozidi kuongezeka, huku wakiathirika kiafya na hata katika ufanisi wa kazi zao. Neno la leo, linatuongoza kumtegemea Yesu Kristo wakati wote tunapopitia changamoto zenye machungu na kuumiza mioyo yetu.

Wengi ni mashahidi kuwa AMANI ya kweli na ya kudumu, inapatikana kwa Mungu. Kuna waliojijengea wigo wa Amani kwa wapenzi wao, mara walishangaa wakipitia machungu baada ya kujeruhiwa na waliokuwa wanawaamini. Hakuna kitu chochote kinachoweza kutupatia AMANI ya kudumu nje ya Mungu.

Hebu kila mmoja wetu aweke Imani yake kwa Mungu, usiruhusu mwanadamu mwenzio abebe nafsi yako, wala pesa isishike nafsi yako, wala kitu chochote, hivyo vyote vinabadilika bila kutarajia. Upendo wa mwanadamu kwako unaweza kutoweka na kuhamia kwa mwingine, lakini Upendo wa Mungu kwako ni wa milele. Mwamini na Kumtegemea Mungu, naye ataujaza moyo wako Amani Kamilifu, mawimbi yakipita HUTAFADHAIKA.

AMANI YA KRISTO IKAIJAZE MIOYO YETU FURAHA NA TUMAINI DAIMA.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299. Kwa ushauri na maombi.





****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA