Saturday, June 11, 2016

  Hayo yamesemwa leo katika ibada kuu iliyofanyika katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Dodoma Kati.
Unaposema suala la unyenyekevu limekuwa ni suala gumu kwa baadhi ya watu katika jamii yetu hasa ya sasa, lakini pia Mungu anawatu wake ambao ni wanyenyekevu.
Hivyo hata tukiwa ni wenye nafasi kubwa kwenye nyanja fulani ndani ya jamii tukumbuke kunyenyekea kwa wengine na tuondoe kujikweza na hivyo tumuachie Bwana yeye ndiye atatuinua kwa wakati wake.
Mahubiri ya siku ya leo yaliletwa na Prince Bahati ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati na akikazia somo lake alitoa mfamo kwa kuwaita viongozi na waandaji wa Mkutano wa Tain Mchungaji Ungani na Mr. Msambwa ambao walipewa kila mmoja maji ndani ya glasi na kukimbia nayo kwenda kwa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Kaskazi mwa Tanzania wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Mchungaji Dr. Godwin Lekundayo na wa kwanza ndiye alishinda zoezi hilo.
Mfano huo ulimanisha kuwa Mungu anapogawa mibaraka kwa mtu hagawi tu bila utaratibu, kwani kwenye zoezi hilo maji yalikuwa yanamwagika na hata kufika yakiwa machache




Kushoto ni Mnenaji wa hubiri la leo Mr. Prince Bahati akiwa na Mfasiri wake Mchungaji Mika (kulia)
Kushoto ni Mnenaji wa hubiri la leo Mr. Prince Bahati akiwa na Mfasiri wake Mchungaji Mika (kulia)
Sindano la kutembea na maji kwa haraka kwenda kwa Mchungaji Lekundayo.
Safari hatimaye Mr. Msambwa(kulia) akiwa ni mshindi wa zoezi hilo kwa kufikisha mapema maji kwa Mchungaji Lekundayo.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA