Monday, June 06, 2016

Waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Mh. Angela Kairuki Akifungua Rasmi mkutano wa TAiN Unao endelea hapa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Dodoma kati lililopo Mjini Dodoma.
Waziri huyu akijibu Ombi la kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania juu ya Ombi la Kupewa siku Mbadala ya Usafi kwani Jumamosi ni siku ya ibada kwa Kanisa hili Waziri alisema Serikali itahakikisha uhuru wa kuabudu kwa madhehebu yote na lamuhimu katika siku hii ni usafi hivyo kwasababu jumamosi mko kanisani basi Waumini wahakikishe Jumamosi mazingira yao yote yanakuwa safi kabla ya sabato kama kawaida ya Waadventista WA sabato huandaa sabato mapema.
Waziri ametoa Rai kwa Wana TAiN na Kanisa la Waadventista kwa ujumla kuzingatia Maadili ya Matumizi sahihi ya mitandao mbalimbali ya habari kulingana na Sheria ya mtandao na habari.
Mikutano hii iliyo anza jana tarehe 05/06/2016 itaendelea hadi jumamosi ya tarehe 11/06/2016
Jopo la maafisa wa kanisa walipokuwa wakifatilia hotuba ya Waziri Angela Kairuki (hayupo pichani)
 Picha& Habari na  Haruni Kikiwa



****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA