Tuesday, August 23, 2016

Yesu, kama Bwana, aliwajua watu Zaidi yalivyokuwa wakijifahamu wao wenyewe. Kuna maelezo mengi katika injili ambapo Yesu alionyesha kwamba sio tu alijua walichokuwa wakifikiri kwa wakati huo ( soma Marko 2:8)- Yeye alijua historia zao pia ( Yohana 4:18)

Soma Zaburi 139:1-13. Neno la Mungu linatwambia nini hapa?
Kama tulivyoona jana, Yesu alikuwa anayatambua mahitaji ya watu, na alihudumu kwaajili ya mahitaji hayo, Ki ukweli aliyatambua hata mahitaji yaliyokuwa chini ya uso wa dunia, ukweli huu unadhirika katika kisa cha mtu yule aliyekuwa amepooza. Ingawa ilikuwa inaonekana dhahiri kwamba alihitaji uponyaji wa kimwili, kulikuwa na jambo kubwa Zaidi pale, ambacho hata kabla ya kumwambia ajitwike godoro lake na kwenda, “Yesu alisema mwanangu umesamehewa dhambi zako” ( Marko 2:5).

Soma Marko 2:1-12. Ni nini kilichokuwa kinaendelea ndani ya mwanaume huyu? Ni kwa njia gani hitaji hili la ndani, laweza kuwa tatizo kwa wale tunao wahudumia?
Yesu alitambua kwamba tatizo pale lilikuwa ni Zaidi ya ugonjwa. “Hata hivyo haukuwa uponyaji wa kimwili ( kwa yule mwenye kupooza) alitaka msaada sana katika mzigo wa dhambi. Kama angeweza kumwona Yesu na kupokea hakikisho la msamaha wa dhambi na kuwa na Amani na mbingu, Angekubali kuendelea kuishi au kufa. Kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu”-Ellen G.White, The Desire of Ages,uk.267.

Bila shaka sisi hatuwezi kwenda kwa undani kama Yesu alivyofanya. Hata hivyo tunaweza kuwa na uhakika kwamba wale wote ambao tunawahudumia, ni viumbe walio haribiwa na dhambi, hiyo ni kusema pamoja na mahitaji yao mengine wao pia wanahitaji neema ya uhakika, ya maarifa kwamba yuko Mungu anayewapenda na aliyekufa kwa ajili yao na anayewatakia yaliyo mema pekee.

Fikiria ni kwa kiasi gani unatamani kupata uhakika wa wokovu na wa maarifa kwamba Mungu anakupenda. Unawezaje kuwasaidia wengine kupata uzoefu na uhakika wa upendo huo?

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA