Tuesday, December 13, 2016

 Mithali 16:25 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti."

Wapendwa tunaishi nyakati mbaya sana, nyakati za usiku wa giza nene, wengi wana macho lakini yameshapofuka hayaoni, na wengi wana masikio lakini yamejaa matope wala hawasikii. Wengi wanakufa ghafla bila matumaini.

Hebu jiulize! Ni kweli watu hawazisomi na kuzielewa AMRI za Mungu, Kama zilivyoandikwa kwa ujumla katika, Kutoka 20:1-17?  Je ni kweli watu hawajui kazi aliyokuja kuifanya Yesu kama ya KUOKOA (Kuwapatia Ushindi wa Dhambi), Mathayo 1:21?

Kama kweli vijana na wazee wana macho yanayo ona, na masikio yasiyo na matope; Uzinifu na Uasherati unatoka wapi? Majungu, maneno ya hila na Uongo, hisia mbaya, ulevi, visasi, uonevu, vinatoka wapi?, bila kusahau kwenda kwa waganga wa umizimu kutafuta ulinzi na kuondoa mikosi, kuitumia siku ya SABA ya juma kinyume na agizo la Mungu na mafundisho ya Yesu, na kuwa ndiyo siku ya Starehe, Sherehe na kila ufisadi na uchafu?.

Wakati Shetani anatangaza Ushindi, kwa kuwajeruhi wengi na kuwachukua mateka, akitumia umizimu na manabii, mitume, walimu na watumishi kwa udanganyifu juu ya kweli ya Mungu; Bado tumaini la kuokolewa lipo - FANYA UAMUZI LEO. Hebu kila mmoja aithibitishe imani yake kwa neno la Kweli la Mungu.

Hizi ni nyakati za mwisho: Mungu ambariki kila mmoja anapozitafakari njia zake na kufanya UAMUZI SAHIHI.

NAWATAKIA JUMATANO NJEMA, IWE YA BARAKA TELE.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299 - Email... Eliezer.mwangosi@yahoo.com.



****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA