Friday, January 27, 2017




Waebrania 4:12 "Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."

Ni kawaida ya binadamu kupenda kuambiwa mambo mazuri, yanayofurahisha moyo, mfano kusifiwa au kuambiwa maneno yasiyokinzana na matakwa yake. Watu wengi wanachukia wanapoambiwa ukweli ili wajirekebishe wanapokosea, ndio maana waswahili wakaishia kusema "UKWELI UNAUMA". Iwe ofisini, kwenye biashara, majumbani watu hawapendi kukosolewa, au kambiwa ukweli pale wanapokwenda tofauti.

Kwa bahati mbaya sana tabia hii imetanda hata kwa watu wanaodai ni watu wa Mungu, katika kizazi hiki cha giza nene la mioyo iliyojaa uovu, watu hawapendi kuambiwa neno la Mungu linalokosoa tabia zao zilizo kinyume na mapenzi ya Mungu, wengi wanapenda maneno laini,  vichekesho, baraka, mafanikio na yanayofanana na hayo. Neno la maonyo na kukemea dhambi linazidi kuadimika masikioni mwa wanadamu.

Hata kwenye mitandao, mtu akirusha ujumbe wa kidunia, mfano: Binti akapiga picha yenye kuacha embe dodo nusu wazi, au akaonyesha maungo ya makalio, hata kama ni ya kuazima kwa wachina, halafu akaandika na ujumbe usemao "Sema neno moja tu", utashangaa comment zikimiminika utafikiri mvua. Lakini mtu akituma ujumbe wenye kuleta uzima, wanapita au ana bofya "like" bila hata kusoma na kutafakari.

Kazi ya neno ni kufanya "operation" au upasuaji ili kugawanya mwili (nafsi) na roho, yaani kukata na kutupa nje mazoea ya mwili na kuunganisha tabia ya Kristo kwa njia ya Roho mtakatifu. Sijawahi kuona mtu akifanyiwa upasuaji, katika machungu ya kisu, eti anacheka mwanzo mwisho, au mtu anameza dawa ya chloroquine huku anacheka. Lakini siku hizi,  mahubiri mengi na yanayopendwa na wengi ni ya wenye dhambi kurudi nyumbani na dhambi zao, huku wakidai wamebarikiwa kwa vichekesho na jumbe laini za baraka. Lengo la wahubiri wengi ni kutaka kupendwa na kujikusanyia sadaka, huku watu wakibaki chini uovu.

Zingatia: Ukiona umehubiriwa na umesikia au umesoma neno la Mungu, na ukaona liko tofauti na unayopenda kuyafanya, au linakosoa unachokiamini, na ukasikia kuumia moyoni, unapaswa kumshukuru Mungu, hilo ndilo lengo la neno la Mungu. Ulimwengu unazidi kuwa chini ya laana ya dhambi, kwa sababu watu hawako tayari kuonywa na kuambiwa ukweli kupitia neno la Mungu.

HEBU MUNGU AMSAIDIE KILA MMOJA AWEZE KUSHINDA

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUJAA BARAKA ZA BWANA.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299 na WhatsApp - 0766992265.






****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA