Thursday, January 12, 2017

Ni mara ngapi umejaribu kuweka wakfu talanta uliyopewa na Mungu kwa ajili ya kulitukuza jina lake?
Mara ngapi umeweka ahadi au nadhili kwa Mungu kupitia kile alichokupa?
ni mara ngapi umetimiza nadhili hiyo na ukafanya tathmini na kupata majibu sahihi ya kile ulicho ahidi?
Tarehe na mwezi kama huu, mwaka 2013, Kijana anayetokea katika familia ya uimbaji ya Mwalimu Mgini Kweba, Josee Ndaro Kweba alitoa wazi wazi kile kilicho moyoni mwake baada ya kuandika "I want to Use my hands in Praising the Lord SooN My Dream will come true God help me" akiwa na maana (Nahitaji kutumia mikono yangu katika kumtukuza BWANA, karibuni njozi yangu itakuwa kweli, MUNGU nisaidie).
Ni ukweli usiopingika kwamba uwezo wake wa kupiga kinanda umekuwa ukiendelea kukuwa siku hadi siku kwani hadi sasa amekuwa akionekana katika matukio tofauti tofauti ya kumtukuza mungu kwa kutumia mikono yake.
Je, ni kwasababu ya nia, ahadi na ombi alilomuomba Mungu miaka minne(4) iliyopita...?
Timu nzima ya injilileo blog, tunaendelea kumuombea kwa Mungu, ili kupitia huduma yake watu wengi wapate kumuona Bwana. Amina!

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA