Monday, January 09, 2017

Michael Jordan alizaliwa mwaka 1963, katika makazi duni ya Brooklyn, New York.
Alikuwa na ndugu wanne na mapato ya baba yake hayakuwa ya kutosha kwa ajili ya familia nzima. Yeye alikulia katika kitongoji maskini. Akitokea katika eneo lenye vurugu na ubaguzi mzito katika makazi duni, hakuona tumaini lake la baadaye.
Baba yake aliona katika Michael, nafsi iliyopotea na kuamua kufanya kitu.
Alimpa Michael, aliyekuwa na umri wa miaka 13, kipande cha nguo kilichokwisha kutumika na akamuuliuliza: "Je, unafikiri thamani ya hii nguo itakuwa kiasi gani?"
Jordan alijibu, "Labda dola moja".
Baba yake aliuliza, "Je, unaweza kuuza kwa dola mbili? Kama utaweza kuuza, itakuwa na maana kwamba wewe ni msaada mkubwa kwa familia yako."
Jordan alitikisa kichwa chake, "Nitajaribu, lakini hakuna uhakika kwamba mimi nitafanikiwa." Jordan kwa umakini alisafisha nguo kuwa safi. Kwa sababu hawakuwa na Pasi, aliitandaza katika kipande cha ubao kilichonyooka na baadaye akaiweka juani ili ipate kukauka.
Siku ya pili, alienda na ile nguo katika sehemu yenye msongamano wa watu katika Kituo cha Usafiri cha chini ya ardhi. Baada ya kuinadi hiyo nguo kwa zaidi ya masaa sita. Jordan hatimaye aliweza kuuza kwa $ 2. Na alichukua kiasi hicho cha fedha na kuelekea nyumbani kwa haraka.
Baada ya hapo, kila siku alikuwa akichukua mavazi yaliyokwisha kutumika, na kisha kuyaandaa vizuri, na kuuza katika umati wa watu.
Zaidi ya siku kumi baadaye, baba yake tena akampa nguo iliyotumika, "Je, unaweza kufikiria njia ya kuuza hii kwa zaidi ya ile?"
Jordan alisema kwa kulalama, "Itawezekanaje? Hii nguo inaweza tu kuuzwa si zaidi ya dola mbili" Baba yake akajibu, "Kwanini usijaribu kwanza? Kunaweza kuwa na njia."
Baada ya kuumiza kichwa chake kwa saa kadhaa, hatimaye, Jordan alipata wazo.
Alimuomba binamu yake amsaidie kuweka picha ya Donald Duck na Mickey Mouse katika lile vazi. Kisha alijaribu kuuza katika shule ambapo watoto wa kitajiri wanasoma.
Mara Msaidizi wa Nyumbani, ambaye alikuwepo katika eneo lile kumchukua bwana wake, alinunua ile nguo kwa ajili ya bwana wake. Bwana wake alikuwa kijana mdogo wa miaka 10 tu. Yeye aliipenda sana ile nguo hivyo akatoa dola ishirini na tano. Dola 25 ilikuwa kiasi kikubwa kwa Jordan, sawa ya mshahara wa mwezi mmoja wa baba yake.
Alipofika nyumbani, baba yake alimpa tena nguo nyingine iliyotumika, "Je, unaweza kuiuza kwa bei ya dola 200?" 
Wakati huu, Jordan alikubali nguo bila shaka hata kidogo. Miezi miwili baadaye mwigizaji mmoja maarufu wa Sinema ya "Charlie's Angels", Farah Fawcett alikuja New York kwa ajili ya kuitangaza Sinema yake hiyo.
Baada ya mkutano na waandishi wa habari, Jordan alifanya njia yake kwa kwa kuwapita vikosi vya usalama kufikia upande wa Farah Fawcett na kumumba aweke Saini ya jina lake juu ya nguo ile. Baada ya Fawcett kumuona yule mtoto mdogo asiye na hatia kuomba kuwekewa saini yake, yeye kwa furaha alisaini juu ya ile nguo.
Jordan alikuwa akipiga kelele sana, "Hii ni jezi iliyosainiwa na Miss Farah Fawcett, bei ya kuuzia ni dola 200!".
Aliendesha mnada, kwa mfanyabiashara kwa bei ya dola 1,200!
Aliporudi nyumbani, baba yake alidondosha MACHOZI na kusema, "Mimi nimeshangazwa kwamba umeweza kufanya hivyo mwanangu! Wewe ni mkubwa kweli kweli!"
Usiku huo, Jordan alilala pembeni ya baba yake.
Baba yake alimuuliza, "Mwanangu, katika uzoefu wako wa kuuza vipande hivyo vitatu vya mavazi, nini wewe umejifunza kuhusu mafanikio?". Jordan alijibu, "Penye nia, pana njia". baba yake alitikisa kichwa chake, kisha kisha akainua kichwa chake akamwambia, "Hicho ulichokisea ni sahihi! Lakini hiyo haikuwa nia yangu. nilitaka tu kuonyesha kwamba kama kipande cha nguo kilichotumika ambacho kina thamani tu dola pia kinaweza kuongezeka katika thamani, Basi vipi kuhusu sisi tunaoishi na tuna akili ya kufikiria?; tunaweza kuwa weusi na maskini, lakini vipi kama sisi tungeweza  kuongeza thamani yetu".
Hii ilileta mwanga kwa kijana Jordan. Kama kipande cha nguo kilichokwisha tumika kinaweza kuwa na heshima, kwa nini basi si mimi? Hakuna kabisa sababu ya kujishusha mwenyewe.
Kutokea hapo, Michael Jordan aliona kuwa mustakabali wa maisha yake utakuwa mzuri na uliojaa matumaini.
Aliendelea hivyo na kuwa mchezaji bora katika mpira wa kikapu, kwa nyakati zote.
Ninawezaje kuongeza thamani yangu mwenyewe?

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA