Friday, January 20, 2017

Peter akiwa Studio katika maandalizi ya moja ya kazi zake
Muimbaji, Peter Joseph
Muimbaji wa nyimbo za Injili na katika kikundi cha uimbaji cha The Holy Reunion na ambaye pia amewahi kuwa mshindi wa tuzo za Glorious Music Awards zilizoandaliwa na kituo cha Runinga cha Morning Star, Peter Joseph, usiku wa leo amempoteza mama yake Mzazi Bi. Joyce Petro katika Hospitali ya wilaya ya Misungwi jijini Mwanza.

Marehemu Bi. Joyce hadi mauti ilipomkuta usiku wa tarehe 20/01/2017 amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kiharusi na Shinikizo la damu(BP).

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumapili ya Tarehe 22/01/2017 huko Nkorati, Misungwi jijini Mwanza.

Injilileo blog, itaendelea kukutaarifu kila taarifa inapokuwa imetufikia.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE! 

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA