Dalili
kubwa ya hatua hii ni upele. Vipele huanzia upande mmoja wa mwili na
kuenea sehemu zingine za mwili. Vipele hivi hujitokeza kuanzia wakati
ambao kidonda kinapokuwa kinapona na vinaendele majuma mengine hata
baada ya kidonda kuwa kimepona na vinakuwa haviwashi.
Hatua ya mbali( late stage).
Hatua hii hufuata baada ya hatua hizo hapo juu kuwa zimekwisha. Endapo
mgonjwa hakutibiwa huendelea kuw na wadudu kwenye damu hata kama hana
dalili. Dalili zake ni kushindwa kutumia viungo, upofu, kufanga ganzi na
kupoteza kumbukumbu.
Maambukizi
Kaswende huambukizwa endapo majimaji ya kwenye kidonda hugusana na
mwili. Lakini pia huambukizwa kwa njia ya ngono, na hata kunyonya mate
na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Vipimo
Muda mfipi baada ya kupata maambukizi mwili hutengeneza kinga ya
kupambana na wadudu wa kaswende. Hivyo hii kinga inaweza kupimwa
maabara kwa kutumia kipimo maalumu. Wakati mwingine uchunguzi huwezwa
kufanya kwa kuchukua majimaji kutoka kwenye kidonda.
Uhusiano kati ya kaswende na HIV
Kwakuwa mgonjwa wa kaswende anakuwa na vidonda ni rahisi kupata maambukizi ya HIV.
Matibabu.
Hakuna matibabu ya nyumbani yanayoweza kuponyesha huu ugonjwa. lakini
unatibika kwa urahisi kwa kutumia antibiotics amabazo unaandika na
daktari. Hivyo unapokuwa na dalili hizo ni vyema kuwahi hospitali,
www.masua.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment