Sunday, March 31, 2013
ENOCK NKAINA msemaji toka SUA aimbia blog yetu: Tulikuwa na vipindi vya mafundisho ya watoto na kama watoto wangekuwa wanabatizwa tungepata kundi kubwa mno kama uonavyo. Lakini pia tulikuwa na wahudumu watatu wa mkutano, wakiwemo watumishi wawili kutoka AMR yaani Adventist and Muslims Relations, waliichambua Biblia pamoja na Quran kwa undani zaidi. Kitu tulichojifunza hasa, ni kuwa hata ndani ya Quran utunzaji wa sabato umesisitizwa sana. Lakini pia utamuona mzee mmoja hapo akihubiri, anaitwa Mwinjilisti, Fadhili Ngomoi. Yeye ndiye aliyekuwa mhututbu mkuu. Alitupa mafundisho mazuri na makubwa kwakweli. Zaidi ya yote, Tunamshukuru MUNGU kuwa, baada ya wiki mbili za mkutano,watu 16 waliamini ukweli na kubatizwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment