HEBU POKEA TAARIFA HII KUTOKA KWA PR. MUSA MIKA AMBAYE NI
MKURUGENZI WA VYOMBO VYA HABARI VYA KANISA LA WA ADVENTISTA WA SABATO
TANZANIA.
UZINDUZI WA TELEVISHENI YA MORNING STAR
Tunamshukuru sana Mungu kwa kuwezesha upatikanaji wa lesseni ya televisheni ya Morning Star.
Aina ya lesseni tuliyopewa ni ya kurusha matangazo katika mkoa mmoja tu
wa Dar es salaam. Hata hivyo kwa ushirikiano na HOPE CHANNEL baada ya
kushauriana na Mamlaka Ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania matangazo
yale yale ya Morning Star TV yanaweza kurushwa kupitia Televisheni ya
Hope. Tunakusudia kurusha matangazo ya Morning Star Televisheni Dar es
salaam (ambayo pia yanatarajiwa kuonekana Arusha, Dodoma, na Mwanza) na
pia kote nchini inakoonekana STAR TIMES kupitia Televisheni ya Hope.
KISEMBUZI(DECODER)
Aina ya King’amuzi (kisembuzi) tutakachotumia ni DigiTek Kwa Dar es
salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha, pamoja na STAR TIMES kwa sehemu zote
inakofika nchini inakofika Star Times. Kwa sasa Star Times wamefika
mikoa Kumi na Nne.
Kwa mkoa wa Dar es salaam tutarusha
matangazo moja kwa moja, mtazamaji atapokea matangazo kupitia DigiTek.
Kwa mikoa mingine nje ya Dar es salaam Matangazo yetu yataonekana
kupitia Hope Channel ambayo itakuwepo kwenye Kisembuzi cha Star Times
lakini kwa masharti ya Mamlaka ya Mawasiliano Southern Highlands Conference of SDA Church-TANZANIA
mtazamaji atalipia kifurushi cha shilingi ishirini elfu kwa mwezi ili
kuyaona. Hii ni kwa vile Hope Channel kiasilia ni televisheni ya
satellite. Sisi tunaona hii ni afadhali mno kuliko kusubiri mpaka
tutakapo pewa lesseni ya kwenda nchi nzima.
Urushaji wa
Matangazo ya Televisheni ya Morning Star kwa Dar es salaam utagharimu
dola za marekani elfu ishirini na nne kwa mwaka. Urushaji Kupitia Hope
Channel Utagharimu Dola za kimarekani laki moja na ishirini na nne elfu
kwa mwaka. Gharama za vifaa vya kurushia pamoja na ufungaji wake ni
Dola za Marekani elfu thelathini na sita.
Kitarakimu ni kama ifuatavyo.
1. Gharama za kurusha Matangazo Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, na Arusha 24,000 USD
2. Satellite uplink charges 100,000USD
3. Service Charges 24,000USD
Jumla USD184,000
Jumla kwa Shilingi za Tanzania ni Tshs 301,760,000
Tumepanga kwamba Uzinduzi wa Televisheni ya Morning Star Ufanyike
tarehe 19.04. 2014 katika viwanja vya sabasaba Dar es salaam. Mgeni
Rasmi ni Dr Benjamin Shoun, Makamu Mkuu wa Mwenyekiti wa GC, Mwenyekiti
wa Divisheni yetu Mch. Blasious Ruguri, Maofisa Wakuu wa Hope
Ulimwenguni, Wenyeviti wa Union zetu mbili. Mgeni rasmi wa kiserikali
anayealikwa ni Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Ili kufanikisha shughuli hii nyeti Unioni zetu mbili zitachangia kwa mchanganuo ufuatao:
Unioni ya Kusini (STU)
STU – 5,000,000
SHC - 8,000,000
ETC- 19,000,000
TAP- 3,000,000
HHES- 2,000,000
Kwa upande wa Sadaka zitakazotoka kwa washiriki wakati wa ibada tarehe 19.04.2014 mchanganuo wake utakuwa hivi:
SHC- Sh. 30,000,000 (Milioni thelathini)
ETC- Sh. 53,000,000 (Million Hamsini)
Jumla kuu 120, 000,000
Union Konferensi ya Kaskazini (NTUC)
NTUC - 8,000,000
NETC- 11,000,000
SNC- 10,000,000
MC- 4,000,000
WTF- 3,000,000
Kwa upande wa Sadaka zitakazotoka kwa washiriki wakati wa ibada tarehe 19.04.2014 mchanganuo wake utakuwa hivi:
MC- Sh. 30,000,000( milioni thelathini tu)
WTF- sh 30,000,000 (milioni thelathini tu)
NETC- sh 40, 000,000 (million arobaini tu)
SNC- sh. 44,000,000 (milioni arobaini na nne tu)
Jumla Kuu 200,000,000.(milioni mia mbili tu)
Mchanganuo uliotumika hapo juu kwa conferensi na taasisi ni wa zile
ahadi ambazo hazikutekelezwa mwaka jana hata baada ya kupitishwa na
kamati kuu ya TUM.
Siku ya Uzinduzi kutakuwa na somo maalum
litakalo tumwa kwenu juma lijalo ambalo litafuatiwa na sadaka maalumu
nchi nzima kwa ajili ya Televisheni ya Morning Star.
Hata hivyo
Tanzania Adventist Media inaandaa Tshirts Maalum zitakazo uzwa kwa
ajili ya kuvaliwa nchi nzima siku ile ya uzinduzi, Taratibu zingine
tutazileta kwenu hivi karibuni. Bwana awajalie neema yake tunapoelekea
mwanzo huu mkubwa wa matumizi ya chombo hiki cha utume.
UJUMBE KUTOKA SHC
NDUNGU WAAMINI WOTE WA SHC NA TANZANIA YOTE KWA UJUMLA HEBU TUTOE
KWAAJILI YA MAPUNGUFU HAYA. KUMBUKA KUTOA KWA KAZI YA MUNGU NI
KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI
MAMBO MAWILI YA MUHIMU
1.
KWA WAAMINI WOTE WA SHC TUMETOA MAGOLI KWA KILA KANISA HEBU TOA KWA
WINGI ILI KUHAKIKISHA GOLI LENU MMEVUKA NA BWANA ATAWABARIKI.
2. KWA
WASIYO WAAMINI HEBU TOA MCHANGO WAKO KWA NAMBA AMBAZO NIME ZIWEKA HAPO
KATIKA PICHA NA BWANA AKUBARIKI KWANI HII TV SI YA WAADVENTISTA WA
SABATO TU BALI NI KWA AJILI YA WASAFIRI WOTE WAKWENDA MBINGUNI HAPA NI
PAMOJA NA WEWE.
BARIKIWA SANA KWA KUIBARIKI KAZI YA BWANA
FROM
PR. HARUNI N.E KIKIWA
COMMUNICATION DIRECTOR
SOUTHERN HIGHLANDS CONFERENCE
*************MATH 28:19-20 "BASI ENENDENI...''*************
0 comments:
Post a Comment