Friday, April 04, 2014


Baadhi ya wachungaji wakiwa kwenye msiba wa pastor Godson


wanakwaya wakiwa kwenye msiba wa pastor Godsoni

Pastor Tuvako pia nae aliweza hudhuria msiba huo


Hili ndilo jeneza la Pastor Godsoni Elieneza
Pastor Godson akiagwa na Wapendwa wake Huko Hedaru



HISTORIA YA PR GODSON
Historia fupi ya Pr Godson Mariatabu Elieneza alizaliwa mnamo 14 Sep 1925 huko Ntambwe Mizirembwe Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa 1 kati ya watoto 12 wa mzee Elieneza Lushino.Alifunga ndoa na Mama Sister Andrea Mburuja Mwaka 1949.Hawakujaliwa kupata mtoto.Alisoma shule ya msingi Vugwama na Suji mwaka 1938 hadi 1946 baada ya hapo alijiunga na chuo cha ualimu Ikizu mwaka 1947 na mwaka huo huo alihamia Bugema kwa masomo ya kichungaji na mwaka 1962 alianza stashahada ya uongozi katika chuo cha Solus Bulawayo Zimbabwe.Pr alipata ubatizo mwaka 1943 katika kanisa la Suji SDA na hadi anafariki ushirika wake upo katika kanisa la Bethlehem SDA Hedaru.Ametumika kanisani kwa zaidi ya miaka 42.Aliwahi kuwa chaplensia wa Ikizu,,Pr wa mtaa wa Makanya na Aliwekewa mikono mwaka 1961.Pr Godson alienda Mwanza kama mmishenari na ni miongoni mwa Wainjilisti wa kwanza kupeleka injili ya SDA katika mkoa wa Mwanza.Pr aliwahi kuongoza idara mbali mbali za kanisa kama vile,,Elimu,,Uchapaji na Vijana na alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Field Cconfrence kwa miaka 15.Baada ya kustaafu aliendelea kutumikia jamii kwa huduma za kiroho kama Mshauri,,Muombeaji na Mpatanishi wa makosa mbali mbali ya kijamii pia Pr alikuwa ni Mkulima na Mfugaji.Pr anatajwa kuwa Shujaa wa Imani hususani kwa jamii ya Wapare kutokana na mfumo wa maisha yake na muonekano wake katika jamii.Pr anazikwa leo Huko Hedaru Nyumbani kwake.Jina la Bwana Libarikiwe.

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA