Monday, August 11, 2014

Hatimaye maandalizi ya mkutano mkubwa wa kanisa la Waadventista wasabato maarufu kwa jina la "Mission Extra Vaganza" yaanza rasmi kwa kutambulishwa kwa kamati za maandalizi ya  mkutano huo.
Kamati za mkutano huu mkubwa wa Divisheni ya Mashariki na Kati (ECD) unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 1-7/02/2015 zilitambulishwa kwa wajumbe waliokutana katika kanisa la waadventista Wasabato Ilala na uongozi wa juu wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania (Southern Tanzania Union Mission, STU) Mch. Magulilo Mwakalonge na Mch. Rabson Nkoko.
Mch. Magulilo Mwakalonge (Mwenyekiti) STU akitoa neno fupi na ufafanuzi  wa tukio hilo kwa wajumbe kutoka katika makanisa mbalimbali.

Mch. Rabson Nkonko (mkurugenzi wa mawasiliano) STU akitambulisha kamati za maandalizi ya mkutano kwa wajumbe. wa kwanza kushoto ni Mch. Shehemba (mchungaji wa kanisa la wasabato Ilala) na wa mwisho Kulia ni Mch. Ungani. Picha na Eliya Marwa.


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA