Monday, August 18, 2014

Mkutano huu umeanza kwa matukio haya,likianza gwaride toka kwa vijana wa Pathfinder(PF) na Adventist youth(AY) kwa kumpokea mgeni rasmi ambaye ni makamu wa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato ulimwenguni Mchungaji Geophrey Mbwana akiwa na Mchungaji Caleb J.Migombo.

Mkutano huu umeanza ukienda sambasamba na muendelezo wa matukio ya uinjilisti wa nyumba kwa nyumba uliofanywa na wakazi wa Mji wa Moshi tangu mwezi 5(tano) na wakazi  hawa ambao pia ni washiriki wa makanisa mama wakifungua madarasa ya kujifunza biblia..

Ufunguzi huu wa mkutano pia ulitoa picha ya ratiba itakavyokuwa kwa siku hizi za mkutano  ambao utakuwa ukianza saa3 asubuhi hadi saa12 jioni ukiwa na vipindi vifuatavyo;-Afya,Computer,Ujasiriamali,Ndoa na familia,Uimbaji na Mfundisho makuu ya imani...

WACHUNGAJI,GEOPHREY MBWANA NA CALEB J.MIGOMBO HAPA WAKIWASILI KATIKA VIWANJA HIVI VYA MASHUJAA SIKU YA UFUNGUZI..
VIJANA WA PATHFINDER WAKIWAVISHA SKAFU VIONGOZI HAWA
MCHUNGAJI MBWANA AKIPEWA MKONO NA KIJANA WA PATHFINDER KATIKA TUKIO LA MAPOKEZI SIKU YA UFUNGUZI..





Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA