Friday, September 26, 2014

Kikundi cha SDA YOUTH ONLINE cha WhatsApp ikimekuwa mbaraka kwa vijana wengi tangu kuanzishwa kwake hadi sana,katika mafanikio ambayo yametokana na mvuto wa mafundisho yake mbalimbali kama vile;-mahusiano,nishani,mapishi,ujasiriamali,lessoni,afya na unabii.
Mafundisho haya yameweza fanyika chini ya walimu na wakufunzi mbalimbali ambao pia wamekuwa msaada kwa kurekebisha na kusaidia kuweka njia mbadala juu ya matatizo ya maswali mbalimbali kwa hawa vijana.
Kutokana na ukubwa wa kikundi hiki,sasa kimegawanywa katika vikundi vidogo vinne yaani A,B,C na D na vikundi hivi vikiwa na waratibu na ratiba ambazo ziko chini ya kiongozi wake mkuu ambae ni Joel Majumbi.
Leo ijumaa ni siku ambayo vijana hawa watakuwa safarini kwenda Zanzibar kwa jukumu la uinjilisti na pia kutakuwa na huduma mbalimbali kama kuchangia damu,ugawaji wa vitabu vya tumaini kuu,kugawa mahitaji ya dawa ya meno,sabauni na miswaki kwa wagonjwa mahosptalini na pia kuingaza nuru ya kweli kwa kuhubiri neno la uzima kwa kutumia Biblia pia na Quruan.
Mawasiliano ni +255715-950-444.+255782-950-444 +255754-950-444
BAADHI YA VIJANA WA SDA YOUTH ONLINE(WhatsApp) WAKIWA KATIKA MAKUTANO YA PAMOJA SIKU YA KUHITIMISHA KAMBI LA MAGOMENI AMBAPO PIA ILIKUWA SIKU MAALUM YA MUJADILI JUU YA SAFARI HII YA ZANZIBAR
PICHANI:KUTOKA KUSHOTO NI JOEL MAJUMBI(KIONGOZI),WILLIAM SINGO,HILDA BASIL,JOHN KAMPA,GLORIOUS NYAKYEMA NA LULU NICHOLUS.

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA