Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni Misheni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji James Machage amewataka washiriki wa kanisa hilo wanaoishi mijini bila kufanya kazi kurudi vijijini na kujihusisha na kazi za kilimo ili kuleta maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla.
Mchungaji Machage ametoa agizo hilo
katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni anapoendesha mkutano wa
juma la uamusho la uwakili lililoanza sabato iliyopita ambapo amesema
inashangaza watu wengi kuishi katika maeneo ya miji mikubwa kama Dar es salaam
na hawana kazi za kufanya hali inayofanya waongeze msongamano wa watu
wakati kuna maeneo makubwa vijijini yanayohitaji kuendelezwa.
Machage amesema kuwa serikali haina
uwezo wa kuwapatia watu wote ajira hivyo inapaswa wananchi watumie elimu
waliyonayo kukabiliana na mazingira na kujipatia maendeleo yao wenyewe huku
akisisitiza kuwa miji yenye msongamano wa watu kama Dar es salaam waishi watu
walio na kazi tayari.
Mchungaji Machage ambaye kitaaluma
ni mtaalamu wa masuala ya anga amesema imefika wakati sasa kwa waumini wa
kanisa kuweka juhudi katika kutumia elimu waliyonayo kufanyakazi kwa bidii na
kujipatia maendeleo binasfi na kusaidia miradi mbalimbali ya kanisa na kama mtu
anaelimu na hana kazi ya kufanya ni vema kuchukua maamuzi ya kwenda kijijini
kulima na si kuishi mjini wakati hana jambo la kufanya.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment