Huduma ya wana wa kike toka kanisa la Kimara sda wameandaa picnic ikiwa na madhumuni ya kubadilishana mawazo na kutakuwa na huduma mbalimbali kama masomo ya ujasiriamali,afya,kuogelea na michezo mbalimbali.Mama Masige ambaye ni mkuu wa huduma ya wana wa kike kanisani Kimara amesema kwa mwaka huu hii ni picnic ya kwanza na ikiwa na utangulizi wa huduma mbalimbali ambazo zimefanywa ya wanawake hawa kama kutembelea wanahuduma wenzao katika familia zao na kutoa semina na mashauri kwa mabinti juu ya kujitambua na hasa katika mahusiano,safari hii inaanza kanisani Kimara saa 3 asubuhi kwa usafiri wa pamoja
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment