Friday, October 03, 2014

Kijana wa Kitanzania aliyetoa maisha yake kwa kiasi kikubwa katika kumtumikia Mungu wa mbinguni aliye hai. Kwa wale ambao wamepata nafasi ya kumfahamu angalau kidogo watakuwa mashahidi kwa huduma yake kwa Mungu.
Kwanza alianza kuonekana katika kanisa la waadventista wasabato Magomeni jijini Dar es Salaam tangu vyama vilivyo katika kanisa lakini pia alihudumu katika kwaya ya kanisa hilo.
Kama hiyo haitoshi ameshiriki katika vyama vya ASSA na THISDASO kwasasa TUCASA kama mwanachama hai na haina ubishi amekuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi kwani pia alihudumu kama kiongozi katika nafasi mbalimbali za chama na pia kama muimbaji na mwalimu wa kwaya katika kwaya ya ASSA kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar (DAPWAZA).
Kwasasa Yared anapatikana katika kanisa la waadventista wasabato Ilala jijini Dar es Salaam akiwa pia ni mwimbaji wa kwaya ya kanisa hilo na kiongozi wa muziki kanisani lakini ili kuhakikisha ameamua kufanya kazi ya Mungu pia ni mwimbaji wa sauti ya nne katika kikundi cha HOLY REUNION cha kanisa hilo.
Akiwa katika kikundi hicho cha kiinjilisti amesimama kumutangaza Mungu kama Muhubiri mkuu katika mikutano ya injili miwili kwasasasa (Ilala mwaka 2013 mwezi wa 8 na Mlimba 2014 mwezi wa 8).
INJILILEO Blog kwa dhati kabisa inapenda kumpongeza yeye binafsi lakini bila kusahau familia yake yote kwa ujumla, kanisa linalomlea, marafiki na jamaa kwa shughuli wanayofanya katika kuhakikisha anaendelea kutumika hivyo. Zaidi tunamuombea kwa Mungu aendelee kumpigania na kumtumia katika huduma hii ya kumaliza kazi yake. Amina!!!
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA