NA MCHUNGAJI ENOC MWAKALINDILILE(http://mwakalindile.weebly.com/yoshua-na-maisha-ya-ushindi-katika-ahadi-ya-mungu-yoshua-15.html)
Awali ya Yote
Karne chache zilizopita Yesu (au Yoshua kwa kiebrania) aliinua sauti yake juu na kwa mshangao akauliza: "Mwana wa Adamu atakaporudi ataikuta imani?" (Luk 18:8). Haraka, na mimi namshangaa muulizaji. Iweje Bwana anayejua yote aoneshe kutokujua? Ni kweli Mwana wa Mungu hajui atakapokuja mara ya pili kama dunia itakuwa na watu wakishikiria imani au la? Na kama Bwana anataka jibu la maelezo, nani mwenye ubavu wa kumfundisha Bwana—Bwana ambaye hazina zote za maarifa zimefichika ndani yake? Kwa vyovyote, Bwana kwa kuuliza hivyo haitaji maelezo toka kichwani bali maamuzi toka moyoni.
Maana ukweli wa hakika ni huu: imani isiyokauka chemi chemi yake yatokea moyoni na si kichwani. Moyo unasema nitakufuata hata kama sijui niendako; nitakutii hata kama sielewi maagizo yako; nitakuamini hata kama ninaona mashaka. Imani inayobubujika toka moyoni humwagika bila kukwama; ije masika kije kiangazi haikomi kutiririka. Nani mwenye imani ya namna hii katika kizazi chetu? Mtu huyo Bwana anamtafuta.
Lakini wengi wa kimpindi cha Yesu walikosa imani ya moyoni kwa Mungu wao. Kichwani walimwelewa Mungu kama mwenye upendo lakini moyoni wengi walimwona kama kiongozi asiyejali watu wake. Kama anawajali kwa nini wakoloni wa kirumi wanakalia nchi yao ya Palestina? Kwa nini kodi juu, maisha magumu; kwa nini waendele kukandamizwa na Mungu anaona?
Yesu akasema hapana. Mungu si kama mnavyomchukulia kichwani. Yeye si kadhi dhalimu ila ni Baba mwenye upendo kuliko baba zenu, mwepesi kuguswa na kuwatetea wanae wanaomlilia mchana na usiku (Luk 18:7). Yesu alijua ugumu wa moyo wa mwanadamu kumchukulia Mungu kama anajali wakati giza la udhalimu limetanda na haki zao wameporwa. Ndipo alipouliza, “Mwana wa Adamu atakaporudi ataikuta imani?”
Kila kizazi kinachokuja ulimwenguni kinakutana na changamoto ya kumwamini au kumtilia Mashaka Mungu. Nyuma kidogo ya kizazi cha Yesu manabii waliwasihii vizazi vya wayahudi waliokuwa mikononi mwa watawala dharimu wa kipagani wamtumainie Mungu hata kama inaonekana Mungu amewatelekeza. Wajumbe wa Mungu waliwawalilia Waisraeli na Wayuda wakisema, “mwaminini Mungu ndipo mtakapofanikiwa” (2 Nyak 20:20). Bahati mbaya wimbo haukusikiwa na hasa katika enzi za waamuzi. Enzi hizo watu waliona mashaka zaidi kuliko sababu za kumtegemea Mungu. Walihoji yu wapi Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo? Walijiuliza kama Mungu wa baba zao ni Mungu wao? Kama Yahwe ni Mungu wao kwa nini asiwaokoe na adui zao? Kwa nini ni mfululizo wa kushindwa na kutawaliwa haukomi hata waishie kuishi kama wageni na wakimbizi kwenye nchi waliyopewa? Katika kizazi cha waamuzi watu walihangaika kupata majibu ya maswali haya kama msafiri aliyebanwa na kiu jangwani. Kama Mwana wa Adamu angekuja katika siku za waamuzi, bila shaka angekutana na uhaba wa kutisha wa imani miongoni mwa watu wake.
Ili kukabiliana na upungufu huu wa imani katika kizazi kilichoishi baada ya Yoshua Mungu alimsukuma mwandishi wa kitabu cha Yoshua asimulie hadithi ya uaminifu wake kwa watu wake. Kwa maneno machache kitabu hiki kinawaongoza wasomaji wake kumwamini Mungu maana anaaminika. Aliwaahidi waisraeli kuwapa nchi na ndicho alichokifanya kwa mkono wa Yoshua. Nchi ya Kaanani wanayoikalia sasa ni ushahidi wa uaminifu wake. Hata sisi leo tukipitia rekodi ya uaminifu wa Mungu katika kitabu hiki tunaweza kupata uhakika wa nguvu kusalia kumwamini Mungu. Na kwa nini tusipitie rekodi hiyo sasa?
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment