NA MCHUNGAJI MWAKALINDILIE
Zaidi ya kulifahamu Neno lake moyoni, kabla hajafaulu Mungu anamtaka Yoshua asiache kuliongelea mdomoni. Anamwambia, “Kitabu hiki cha torati kisondoke kinywani mwako” (Yoshu 1:8). Neno la Mungu kama siri ya mafanikio sio siri ya kutunzwa moyoni kwa choyo bali kuanikwa nje mdomoni. Yeyote anayeitunza atapoteza tu.
Mungu anamwambia Yoshua, huwezi kulielewa neno kama hutaki kuliongelea. Ukiwa na askari wenzako, marafiki zako, raia wako usione haya kukiri neno langu lililo siri ya mafanikio yako. Na hilo ni kwa manufaa yako Yoshua. Kwa kuliongelea unalielewa zaidi na kulikazia zaidi akilini (waulize walimu watakwambia).
Kuliondoa neno la Mungu kinywani ni mwanzo wa kuliondoa mawazoni. Wana habari wanapokoma kuiweka hadithi katika kurasa zao za mbele habari hiyo hutoweka katika vichwa vya wasomaji. Msomaji gazeti hapati hasara kutojadili habari zilizopitwa na wakati, lakini si msomaji wa Neno. Neno la Mungu lina hadithi isiyochuja, atakosaje kuacha kuisoma na kuizungumzia pasipo hasara ya kupoteza siri ya mafanikio yake?
Ninafahamu wapenzi wasiopenda kuzungumzia wapenzi wao. Hataki rafiki zake wajue mpezi wake. Na kama wanamjua, hataki kumsifia mbele yao. Mara nyingi nimeona watu wanamna hiyo walikwisha poteza wapenzi wao moyoni kabla ya kuwapoteza mdomoni. Mungu anamwambia Yoshua njia ya kupoteza mapenzi ya neno la Mungu ni kutolishiriki katika mazungumzo.
Bwana anamwonesha tena namna ya kuhifadhi hazina ya mafanikio anapomwambia,
“ 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.” Yoshua nataka ufaulu hivyo, “Kitabu hiki cha torati kisondoke kinywani mwako”.
Na ukweli huo unabakia hapo hapo:
Taifa linalonyima watu wake uhuru wa kuzungumzia neno la Mungu haliwezi kufanikiwa.
Chuo kinachowanyima fursa wanafunzi wake kulijadili neno la Mungu haliwezi kufanikiwa.
Nyumba isiyo na nafasi kujifunza pamoja neno la Mungu haiwezi kufanikiwa.
Mtu asiyependa kulishuhudia neno la Mungu hawezi kwenda mbali.
Nasikia Mungu akiniambia, rafiki ninajali mafanikio yako, tafadhali, “Kitabu hiki cha torati kisondoke kinywani mwako”.

SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment