Friday, October 10, 2014

Blogu hii tangu kuanzishwa kwake imepata mafanikio hasa pale inapokuwa ikipewa nafasi toka kwa wadau wake ambao huifanya blogu hii kuwa yenye umuhimu kwa wadau wake pale inapoweka habari za wakati za matukio ya uinjilisti.
Injilileo blogu ikiwa na waandishi wake,imefanya mahojiano na Mr.Mazara Edward Matucha ambaye ni mkurugenzi wa kituo hiki cha Morning Star Televisheni na kiongozi sehemu ya utawala,amesema jukumu la kituo hiki ni kuwahabarisha wadau kwa maneno ya matumaini kwa kipindi hiki cha mwisho wa dunia na kuleta vipindi vilivyokatika hali bora ya kutazamwa na rika zote kwa kuleta uponyaji wa familia mbalimbali.
Tangu kuanzishwa kwake kituo hiki kimepata mbaraka kuwa hewani kwa kuonekana takribani mikoa 10 ya nchi ya Tanzania.
Mstv imejipanga kwa vipindi mbalimbali kama vile,kaya na familia,vijana na wakati,ongeza maarifa,mahubiri,nyimbo na vingine vingi,na ikiwa imekaribia asilimia 2 hadi 3 kukamilika kwa kazi ya kurusha matangazo,Mr.Mazara amesema sasa tukio la kumalizia asilimia hizi ni kuwepo na Mstv Big ya 3 ambayo itafanyika tarehe 1 NOVEMBA,2014,kwa ukanda north Tanzania Union Conference na 1NOVERMBA,2015 kwa ukanda wa South Tanzania Union Mission ni hitaji likiwa ni milioni 255
Pichani kutoka kushoto ni mdau aliyekuja kutembelea kituo hiki,nayefuata ni Mchungaji Mashishanga,anayefuata niMr.Mazara Edward Matucha ambaye ni mkurugenzi wa kituo hiki cha Morning Star Televisheni,secretary wa mstv,mwandishi wa injilileo blog na mdau aliyekuja kutembelea studio za mstv.
Mr.Mazara Edward Matucha ambaye ni mkurugenzi wa kituo hiki cha Morning Star Televisheni akiongea na mwandishi wetu Jackson jana ndani ya kituo hicho. 
Mr.Mazara Edward Matucha ambaye ni mkurugenzi wa kituo hiki cha Morning Star Televisheni akiongea na mwandishi wetu Jackson jana ndani ya kituo hicho.
MWANDISHI NDANI YA STUDIO ZA RUNINGA HII YA MSTV,SEHEMU YA AMBAPO HABARI ZITAKUWA ZIKISOMWA NA VIPINDI VIKIRUSHWA TOKEA HAPA..

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA