Monday, November 24, 2014

Siku ya jana ilikuwa ni tukio lililojumuisha furaha,nderemo na vifijo pia bashasha za aina yake kwa kuwekwa wakfu kanisa la kimara na pia hii huonesha jinsi kazi ya Bwana inavyozidi kukuwa na kuenea kwa kasi.
Kuwekwa wakfu kwa kanisa la waadventista wasabato kumewezeshwa na michango ya washiriki wa kanisa na pia kwa ushirikiano na marafiki wa washiriki wa kanisa kwa kutoa kwa moyo michango na kujituma kumefanya kazi hii matunda yake kuonekana sasa,Bwana awabariki sana.
Vijana wa AY walioteuliwa maalum kwa ajili ya kuwavisha skafu viongozi waliowasili katika viwanja vya kanisa wakifanya hivyo,na pichani kutoka kulia ni Joshua Manyama mshiriki wa kanisa la kimara, Mchungaji Mbuti Kusekwa ndiye aliyewezesha kanisa la kimara kutengwa kuwa mtaa,Mchungaji Ebenea Mbulua ndiye alikuwa mchungaji wa mtaa miaka 15 iliyopita wakati kanisa la kimara likisimikwa kuwa kanisa mwaka 1999,Mchungaji Toto Bwire Kusaga amabye ni Mkurugenzi wa uwakili na majengo kwa ukanda wa mashariki mwa Tanzania ,Mchungaji Tirumanywa,Mchungaji Steven Letta ambaye ni Mkurugenzi wa huduma kaya na familia  kwa Unioni ya Kusini mwa Tanzania  na mwisho ni mgeni rasmi ambaye ni Katibu mkuu wa Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania Mchungaji Sadock Bhutoke..
Picha ni Mgeni Rasmi akiwa msafara ambao ni wachungaji na wazee na kanisa la Kimara..
Gwaride lililoandaliwa na vijana wa kimara wakielekea walipo Mgeni rasmi na msafara wake..


Zoezi la kuvalishwa skafu likafika ambapo kulia ni Mchungaji Letta na kushoto Mchungaji Butoke wakivalishwa skafu hapo jana katika viwanja vya kanisa.
Zoezi limekamilika na vijana wanarudi kwa ukakamavu ..



Msafiri akitembea kwa ukakamavu na kuwapa utaratibu Mgeni Rasmi na msafara alioambatana nao siku ya jana. 
Kijana Msafiri mwenye sale ya vijana akiongoza msafara wa Mgeni Rasmi na waliofuatana nao  kuelekea katika eneo ambapo shughuli hii inafanyika
Hatimaye muda ukafika,kijana msafiri akiongoza viongozi na wachungaji hawa katika zoezi la kuweka wakfu kanisa kwa kutoa utaratibu uliokuwa ukifuata..

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA