Katibu mwenza wa Makao makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Dr Rosa Taylor Banks amewataka wahitimu wa vyuo vikuu kuwa wavumilivu ili kufikia malengo ya mafanikio maishani. Akizungumza kwenye mahafali ya nane ya Chuo Kikuu cha Arusha jana Novemba 30 mwaka huu, Dr Banks ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema uvumilivu ni ziadi ya kuwa na elimu,ubunifu,madaraka na utajiri kwani watu wote walio na mafanikio walipitia changamoto mbalimbali lakini walikabiliana nazo kwa kuwa wavumilivu na kusonga mbele bila kukata tamaa.
=======================
Awali akihutubia mamia ya watu waliohudhuria mahafali hiyo chuoni hapo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Arusha Profesa Emanueli Matiku amesema Chuo hicho sasa kina mkakati wa kuanzisha kitivo cha sayansi ya jamii na teknolojia ili kukidhi mahitaji ya jamii ya kitanzania na kuwezesha kupata wanafunzi wengi wanaojiunga na chuo hicho kutokana na mkazo uliotolewa na serikali ya Tanzania katika kuandaa wataalamu wa fani mbalimbali za sayansi. Jumla ya wahitimu 792 walitunukiwa stashahada,shahada za uzamili na shahada katika fani za elimu,dini,,usimamizi wa fedha,usimamizi wa biashara na thiolojia .
 |
| Mwenyekiti wa union konferensi ya kaskazini mwa Tanzania Dr. Godwin Lekundayo akiwa katika sherehe hizi za mahafari.. |
 |
| Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Emanueli Matiku (Kulia)akihutubia |
 |
| Katibu mwenza wa Makao makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Dr Rosa Taylor Banks |
 |
| Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Emanueli Matiku (Kushoto)akisema jambo |
 |
Mwenyekiti wa jimbo la Mashariki mwa Tanzania(Eastern Tanzania Conference) mchungaji Mark Walwa Malekana akiwa katika sherehe za mahafari haya.. picha na The University of Arusha |
0 comments:
Post a Comment