Friday, December 05, 2014

Rais Vladimir Putin amewaonya wananchi wa Urusi kuwa watakabiliwa na wakati mgumu siku za usoni na kuwataka kujitegemea, amesema katika hotuba yake kwa taifa akilihutubia bunge.
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Urusi imeathirika kwa kiasi kikubwa kiuchumi kutokana na kushuka kwa bei za mafuta na vikwazo kutoka nchi za magharibi vilivyowekwa dhidi ya Urusi kwa kujiingiza katika mgogoro wa nchi jirani ya Ukraine.Sarafu ya Urusi ya rouble, ikiwa ishara ya utulivu chini ya utawala wa Bwana Putin, ilipata anguko kubwa la siku moja, Jumatatu kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1998.
Serikali imeonya kuwa Urusi itaingia katika kipindi cha mtuamo mwaka ujao.Akizungumza na mabaraza yote mawili ya bunge la Kremlin, Bwana Putin pia amezishutumu serikali za magharibi kutaka kuiwekea Urusi vikwazo vipya.
Ameeleza kuwa hajutii kulitwaa jimbo la Ukraine la Crimea, akisema eneo hilo lina maana kubwa kwa Urusi.Amesisitiza kuwa mkasa huo kusini mashariki mwa Ukraine umethibitisha sera ya Urusikuwa ilikuwa sahihi lakini amesema Urusi itaheshimu jirani yake Ukraine kama nchi ndugu.
Akizungumza mjini Basel Uswisi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema nchi za magharibi hazitaki vita na Urusi."Hakuna anayenufaika na mvutano huu... Si mtindo wetu au matamanio yetu kuona Urusi ikitengwa kutokana na vitendo vyake yenyewe," amesema Bwana Kerry.





****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA