Friday, January 30, 2015

 Dr.Hersperance Odhiambo amefundisha somo ya usafi wa maji huku akikemea tamaduni za baadhi ya familia juu ya matumizi mabaya ya maji hasa pale wanapokuwa wakinawa kwenye chombo kimoja cha maji kwa matayarisho ya kupata chakula au tunda.
Ameyasema hayo jana katika kipindi cha Afya kanisani Ushindi Sda kwenye mahubiri ya Somo la "Thawabu ya Uadilifu" linaloletwa kila siku saa12:30 saa2:00 usiku na Mchungaji Geoffrey Mbwana .
Dr.Hersperance Othiambo akisema jambo hapo jana wakati wa kipindi cha Afya katika kanisa la Ushindi sda.

Dr.Othiambo amesema usafi wa maji ni muhimu sana kwa afya ya kila mmoja wetu tofauti na hivyo kuna athari nyingi sana zitokanazo na uchafu wa matumizi mabaya ya maji kama magonjwa ya kuharisha na kichocho pia upungufu au kutumia kiwango kidogo cha maji pia husababisha ukosefu wa choo kizuri au kupata choo kigumu.
Alimalizia kwa wito wa kila mmoja wetu kujali usafi na matumizi sahihi ya maji safi na salama kwa kuyachemsha kabla ya kuyatumia,kunawa vizuri na sabuni na maji hayo yawe na kutosha tena sio ya kuchangia mikono na kila mwana jamii au mwanafamilia husika.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA