Mkurugenzi
Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana
cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona namna kinavtumia
mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw. Mchechu
amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa
kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la
Mtukula linapojengwa jingo la kisasa la biashara na NHC ili kuvutia na
kuchochea ukuaji wa biashara katika eneo hilo la mpaka wa Tanzania na
Uganda. Eneo hili ndipo zilipokuwa nyumba ndogondogo zilizojengwa na NHC
na baadaye kuharibiwa na mabomu ya Nduli Iddi Amin alipovamia nchi yetu
mwaka 1978. NHC iliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kulirejeshea
eneo hilo ili kujenga jengo hilo la kibiashara
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua viwanja vya NHC
Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu ikiwa ni
program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za
makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akimpa maelezo Mjumbe wa Bodi ya
NHC Bi Subira Mchumo ya juhudi zinazofanywa na NHC katika Halmashauri
mbalimbali za Wilaya nchini za kuwapatia wananchi makazi bora. Ujumbe
huo ulitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua mradi wa nyumba za
gharama nafuu Wilayani Muleba na kusisitiza matumizi ya malighafi
zinazopatikana katika maeneo husika ili kupunguza gharama za nyumba
hizo.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika Wilaya ya Muleba kwa ajili ya
kuuzia wananchi. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho ya
ukamilishaji.
Msanifu
wa Majengo wa NHC Bw. Kintu akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC
BW. Nehemia Kyando Mchechu ya jengo linalojengwa na NHC eneo la Mtukula
ili kukuza biashara upande wa Tanzania.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ulipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha
Sukari cha Mtibwa kujionea juhudi zinazofanywa na mwekezaji wa kiwanda
hicho katika kutoa ajira kwa watanzania.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Kiongozi wa
kikundi cha vijana kilichoko Wilaya ya Bukoba Mjini waliyofadhiliwa na
NHC mashine za kutengezea matofali ili kujipatia ajira

.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)


0 comments:
Post a Comment