Friday, January 30, 2015

Taasisi ya wanataaluma wadogo yaani,ASSOCIATION OF ADVENTIST YOUNG PROFESSIONALS(AAYP) inakukaribisha wewe mwanachama na usiye mwanachama kuhudhuria hapo kesho katika ibada ya siku ya Sabato ya pamoja itayoanza asubuhi hadi jioni ikiratibiwa na Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati Mchungaji Dr.Blasious Ruguri.
Mchungaji Ruguri anatarajiwa kuzindua taasisi hii rasmi hapo kesho katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ulio karibu na chuo cha IFM-Posta jijini Dar Es Salaam na Mchungaji Ruguri siku inayofuata(jumapili) atakuwa anaweka wakfu kanisa la Ilala sda.
 Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati ya kanisa la waadventista wasabato Mchungaji Dr.Blasious Ruguri.
Katika siku hii kutakuwa na huduma ya uimbaji toka kwa waimbaji mbalimbali kama;Vocapella,Family Music,Acacia singers,Born to Praise na wengine wengi.
Chakula ni kujitegemea hapo muda wa mapumziko ukifika.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA