Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe.Maabad S. Hoja akifafanua jambo wakati
wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipofanya
ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyopata mkopo kutoka Wizara
ya Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Bw. P. Kagimbo,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia
(MB) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad
Mtanda.
Baadhi
ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wakifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa
Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani)
wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa
hiyo jana.
Kushoto
ni mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Dkt. Maua Daftari
akifuatilia taarifa fupi kuhusu Vikundi vilivyokopeshwa kupita Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana iliyosomwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo, Ustawi wa
Jamii na Vijana wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana (hayupo pichani)
jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya
Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Said Mtanda akizungumza
na wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke kamati hiyo ilitofanya ziara ya
kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana katika manispaa hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Maabad S. Hoja na
wamwisho kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.P. Kagimbo
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Manedeleo ya Jamii, na wataalamu kuto
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia taarifa fupi
ya maendeleo ya Temeke Youth Saccoss wakti wa ziara ya kamati hiyo jana
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Temeke Vijana Saccoss Bw. Swaka Abbas akisoma taarifa fupi ya
maendeleo ya Saccoss yao mbele ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii
(hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilifanya ziara
ya kutembelea niradi ya inayoendeshwa na Vijana kupitia Vikundi
vilivyopata mkopo kutoka katika Mfuiko wa Maendeleo ya Vijana.
Bango likionyesha mahali zilipo ofisi za Temeke Vijana Saccoss.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia(kushoto)
na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad
Mtanda (mwenye miwani) wakisikiliza taarifa fupi ya maendeleo y a
Kikundi cha Vijana Waungwana kinachoendesha mradi wa Saloon na
kujishughulisha na kazi za sana ya muziki katika Kata ya Sandali
Manispaa ya Temeke jana wakati wa ziara ya kutembelea Vikundi
vilivyopata mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Vijana uliopo chini ya
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Baadhi
ya Vijana wa Kikundi hicho wakiendelea kutoa huduma kwa wateja wao kama
wailvokutwa na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii jana jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia
akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mandeleo ya Jamii
walipotembelea katika shamba la matikiti linalomilikiwa na Kikundi cha
Vijana cha Sokoine Youth Development cha Somangila - Kigamboni jijini
Dar es Salaam. Mwenye kofia ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Bw, Bike
Jirani,Mwenye miwani ni Mweneyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Said Mtanda,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.P. Kagimbo na mjumbe wa Kamati hiyo
Mhe. Obama. Kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa mkopo wa jumla ya
shilingi milioni tano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mwenyekiti
wa Temeke Vijana Saccoss ambaye pia ni mwanachama wa Kikunsdi cha
Sokoine Youth Development Bw. Swaka Abbas akifafanua namna ambavyo Mkopo
kutoka Mfulo wa Maendeleo ya Vijana,unaoratibiwa na Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo umewawezesha kuanzisha na kumudu gharama za
uendeshaji wa kilimo cha umwagiliaji katika shamba lao la Matikiti
lilipo katika kata ya Somangila, Kigamboni jijini Dar es
Salaam.Mwenyekoti la kijivu ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Mhe. Juma Nkamia(MB) na mwenye miwani ni Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Mhe. Said Mtanda (MB).
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia(MB)
akikagua mpira unaotumika katika umwagilia kwenye shamba la matikiti
linalomilikiwa na Kikundi cha Vijana cha Sokoine Youth Development cha
Somangila - Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya
Bunge ya Maendeleo ya Jamii jana jijini Dar es Salaam.
Picha
ikionyesha miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Matikiti
linalomilikiwa na Kikundi cha Vijana cha Sokoine Youth Development cha
Somangila - Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda (Mwenye
miwani kushoto) akisisitiza jambo kwa mwanachama wa Kikundi cha Sokoine
Youth Development Bw. Swaka Abbas wakati kamati hiyo ilipofanya ziara
ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana katika Manispaa hiyo jana.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

















0 comments:
Post a Comment