Simulizi hizi muhimu itakuwa inakujia kwa siku 3 yaani Jumatano,ijumaa na jumapili.
Imeandaliwa na Mch J.Kuyenga
Historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato katika sehemu za kati,Mashariki,Kusini na magharibi mwa Tanzania.
MWANZO WA UINJILISTI KATIKA TGF
Kupanuka kwa kazi ya injili katika TGF kulikuwa na kiasi kipindi cha Mchungaji Dobias.
Mchungaji Dobias aliyeitwa mwinjilisti wa Union ya Tanzania,kwanza alipelekwa Kibidula kutumika kama Farm Manager.Kazi ya farm manager hakuipenda sana,ndipo akaanza mpango wa kutuma wainjilisti katika maeneo mapya kutoka sehemu kadhaa za Tanganyika.
Programu ya Mch. Dobias ilizalisha wainjilisti waliotumika kama wamishenari wazalendo,ambao walitumiwa sehemu mbalimbali za eneo la TGF,wakiwemo wafuatao;
1.Lameck Mulungu-Njombe
2.Alhpaxad Katogi-Malinyi
3.Rayphord Bulenga-Mpwapwa
Kutokea Dar Es Salaam ambako kazi ilianza kiutume katika maeneo ya kusini Mashariki na kati mwa TFG ya zamani,yaonekana kulikuwepo na mtaa mmoja mkubwa uliochukua mikoa ya Dar Es Salaam,Pwani,Morogoro,Dodoma,Singida kisha kuelekea mikoa ya kusini ya Iringa,Mbeya,Rukwa,Ruvuma,Lindi na Mtwara.Eneo hili lilikuwa kubwa,lenye changamoto kuhudumiwa na mchungaji mmoja,pamoja na kwamba alikuwa na msaada wa wainjilisti wa vitabu au wainjilisti wa kujitolea.
Katika kukabiliana na changamoto ya ukubwa wa eneo uliaanzishwa mtaa wa kusini chini ya uongozi wa Mch.Joshua Kamenya Kajula,wenye makao makuu Mbeya mwaka 1972.Pastor Yohana Lusingu akaingia katika mtaa huu mpya na Pr.Kajula akaendelea hadi Songea.Kazi iliendelea vizuri kusini,nyumba kadhaa zilinunuliwa na Pr.Dobias katika miji mbalimbali kama vile Masasi na Kilosa,zikatumika kama makazi na mahali pa ibada.
Mkakati huu ulikuwa na udhaifu wake.Kiongozi wa mkakati huu alishikilia madaraka mkononi mwake kwa maana kwamba aliweza kumwachishaa kazi mtenda kazi kwa wakati wowote hata bila kungojea uamuzi wa baraza.Matokeo yake wahubiri hawa wa kujitolea walirudishwa nyumbani.Hata hivyo injili iliendelea kwa nguvu kwa misingi ya imani zaidi.
Pastor Elingoth alishikilia uongozi wa T.G.F badala ya Pastor Henning aliyeitwa kwenda G.C kama Publishing Director.Kazi ilkuwa na kupanuka kutoka mashariki,sehemu ya katika ya Tanganyika,kusini hadi magharibi.Pastor Dobias alichaguliwa kuwa President badala ya Elingoth.Kipindi hiki kilikuwa na migogoro ya uongozi sehemu nyingi.Badala ya Pastor Dobias kubadilishwa kusimamia kusimamia uongozi,Pastor Gabriel Mbwana alichaguliwa kusimamia T.G.F.Lakini uchaguzi mkuu wa union ulikuwa umewadia,uongozi wake ulikomaa baada ya kuchagua viongozi upya na kuipanga T.G.F upya.
INAENDELEA JUMAPILI.....
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment