Thursday, January 01, 2015

 Na mwandishi wetu
Katika kuukaribisha mwaka 2015,washiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato Dar Es Salaam wafanya ibada ya pamoja,ni ibada maalum kwa ajili ya kuukaribisha mwaka 2015 ambayo imefanyika siku hii ya leo tarehe 1 January 2015 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni-Dar Es Salaam.
                                              =====================
Pamoja na huduma ya ibada ambayo imefanyika chini ya uongozi wa Kanisa la Magomeni SDA,program za nyimbo pia zimekuwa kivutio kikubwa kwa washiriki hawa toka sehemu mbalimbali ya Tanzania,kwaya kama Magomeni sda,Temeke sda,Mikocheni A sda,Harvesters,Vocapella,The Twins,kikundi cha Esta,Magomeni sda male voice na Magomeni sda female voice na wengine wengi.
                                                   ====================
Mchungaji Jonas Singo
Mchungaji wa mtaa wa Magomeni sda,Jonas Singo amewataka waumini wa kanisa kukaza mwendo na Bwana licha ya magumu na mazito yaliyowakumba na hata kwa masumbufu yote hayo Bwana alikuwa pamoja nao kwani Bwana asinzii wala hachoki,aliendelea kuwatia moyo kuwa wamfanye Mungu kuwa sehemu ya maisha yao katika kuanza mwaka 2015.
Mwisho wa ibada hii waumini hawa walipata kutoa sadaka ya shukrani...

Mchungaji Jonas Singo

                                         ********HERI YA MWAKA MPYA*******


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0789 243 413 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA